2012-12-06 16:26:43

Patriaki Ignatius 1V Hazim amefariki dunia


Patriaki Ignatius IV Hazim, wa Kigiriki Orthodox la Antiokia na Mashariki yote ya Damaska, alifariki dunia Jumatano , Desemba 5, 2012 , mjini Beirut, akiwa na umri wa miaka 91 kwa matatizo ya kiharusi.

Marehemu Patriaki Hazim alizaliwa katika kijiji cha Mhardey Siria karibu Hama, alikulia katika familia mcha Mungu muorthodox, kama lilivyoeleza na gazeti mahalia la kila siku la "L'Orient-Le jour". Na alisoma nchini Lebanon. Pia anakumbukwa kuwa mmoja wa waasisi wa harakati za vijana waorthodox , katika miaka ya 1942.

Alipata daraja la ushemasi mwaka 1945, na kwenda Ufaransa kwa ajili ya masomo ya Liturujia. Na kurudi Lebanon, ambako alianzisha Taasisi ya Liturujia Orthodox, na kuwa gombera wa katika Chuo Kikuu cha Balamand, Amerika ya Lebanon.

Aliteuliwa kuwa Askofu mwaka 1961, kuteuliwa tena miaka tisa baadaye, kuwa Askofu Mkuu wa Latakia Syria. Na Mwezi Julai 1979, Askofu Mkuu Hazim alichaguliwa Patriaki wa Ugiriki ya kiotodosi ya Antiokia na Mashariki yote.

Mungu alilaze roho yake mahali pema - Amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.