2012-12-01 16:56:32

Mwendo mmoja kuelekea muungano wa Kanisa, licha ya njia ndefu na ngumu - Papa


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, kwa ajili ya adhimisho la Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea, Msimamizi wa Upatriaki wa Kiekumene wa Constantinople, alipeleka ujumbe wake kwa Patriaki Bartolomeo I. Siku Kuu iliyoa adhimishwa na Mama Kanisa siku ya Ijumaa iliyopita.

Ujumbe wa Papa uliwasilishwa kwa Patriaki Bartholomeo I, na Kardinali Kurt Koch, Rais Wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristu, aliyeongoza Ujumbe wa Vatican Istanbul kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu hii.

Papa katika salaam hizo, ameonyesha , tumaini lake katika umoja wa kweli na halisi , licha kwamba bado kukamilika, utajengwa katika misingi, si yenye harahara za nadharia za fadhila nyepesi za kibinadamu, lakini juu ya imani moja katika Bwana Yesu Kristo."

Kwenye ujumbe huo kwa Patriaki wa Kiekumene, Bartholomayo I, Papa amehimiza kusonga mbele katiak hali ya kujiamini , katika njia inayolenga kurudisha, umoja kamili." Barabara ambayo mpaka sasa imekuwa na maendeleo mengi muhimu katika kupeleka mbele hatua , ingawa inaweza kuonekana kuwa "ndefu na ngumu.

Kanisa Katoliki limepania kuendelea katika mwelekeo huu –kwa kufarijiwa na sala ya Bwana wetu Yesu Kristo “aliompa Baba, 'wao pia inaweza kuwa wamoja kama wao walivyo, ili kwamba, ulimwengu upate kuamini" (Yohana 17:21) ".


Na Patriaki Bartholomayo I, kwa upande wake katika maadhimisho haya alisema, "njia ya kiekumeni ni haiwezi kubatilishwa," licha ya kuwa ndefu na ngumu. Patriki aliendela alihimiza kazi za majadiliano , yanayotafuta kuonyesha manufaa ya umoja kuliko migawanyiko.

sherehe hizi zilifanyika katika Kanisa Kuu la Kipatriaki la Fanar, mjini Instabul.







All the contents on this site are copyrighted ©.