Msomi Dr Patriaca, apokea tuzo ya Novak ovak A 2012.
Tuzo ya Novak 2012, ambayo hutolewa na Taasisi ya Acton, mwaka huu imenyakuliwa
na Msomi, Dr Giovanni Patriarca , mwalimu katika taasisi na vyuo vya Nuremberg Ujeruman.
Dr Giovanni Patriarca, alipokea tuzo, hivi karibuni kama ilivyoandaliwa na
Chuo Kikuuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas wa Aquinas cha hapa Mjini Roma.
Waliowasilisha
tuzo hiyo ni Padre Robert Sirico, Mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Acton
, pia akiwepo Kishore Jayabara, Mkurugenzi katika Ofisi za Taasisi ya Acton Roma.
Tuzo ya Novak , ambayo iliitwa kwa heshima ya Mwanateolojia na mwanafilosofia
katika masuala ya kijamii , Michael Novak , hutolewa kwa Msomi, aliyefanya bidii
zaidi katika kuendeleza tafiti na mahusiano ya kina, katika utu wa biadamu na umuhimu
wa mipaka ya kiserikali katika uhuru wa kidini na uchumi huria.
Mshindi wa
tuzo hii , hupokea kiasi cha dola 10,000, na pia huwasilisha mada maalum wakati wa
sherehe za kupokea tuzo, mhadhara unaojulikana kwa jina Calihan. Dr Patriaca , katika
mhadara huu wa Calhan, alisisitiza juu ya ukweli wa asili ya kipeo cha uchumi kwa
wakati huu.
Alisema, ingawa kipeo cha sasa katika asili yake, kinasababishwa
na mambo kadhaa ya kiufundi, lakini pia, ni kutokana na mabadiliko kadhaa katika
tabia za maisha ya kijamii na mahusiano kati ya mtu na mtu. Hivyo kunahitajika mabadiliko
mengine , kwa ajili ya kurejesha tena utulivu. Na kwamba kati ya dalili zinazojionyesha
katika mbadiliko ya sasa, ni uwajibikaji wa mtu kwa yeye binafsi, na katika mahusiano
yake na wengine na kazi za umma. Mabadiliko yanayonekana kukuza moyo wa kujitenga
na wengine na kupendelea zaidi ubinafsi .
Alitoa maelezo hayo kwa kurejea
pia kwamba, katika vipindi vyote vya kihistoria , kumekuwa na enzi za ukosefu wa utulivu
na kipindi cha mpito kinachotaguliwa na mabadiliko katika mtazamo wa kiuchumi na
mahusiano ya kijiografia.
Na alionyesha kujali , umuhimu wa kuongeza jitihada
katika kuyatambua leo hii mazingira ya faragha na mitazamo ya kimataifa. Na mabadiliko
haya hutokea kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba , mtu hushindwa kwenda sambamba na mabadiliko
hayo na hivyo hupelekwa himahima bila ya kujitambua na bila ya kuwa na lengo mfano
wa maji ya yanayo tiririka toka mlimani. Na hivyo uhuru wenyewe unakuwa bandia na
huzidiwa na usasa, na hivyo binadamu hupoteza mwelekeo wa maisha yake ya ndani.
Dr. Patriarca pia alitazamisha katika ubabe na njia zisizofaa, katika demokrasia
ya Magharibi, ambayo kwa sasa misingi yake katika baadhi ya haki fulani zinagandamizwa
na kugeuzwa kuwa hoja.
Msomi huyo ameonya mwelekeo wa watu wa ulaya kusahau
mizizI ya utamaduni wao wa tangu kale za kigriki, kirumi, kiyahudi na Kikristo, kwa
kisingizio cha jina la demokrasia katika chaguzi zinazotafuta kuufunika uwazi na kweli,
zilizosimikwa katika utambulisho wa utamaduni wa tangu zama za kale. Pia ameasa
dhdi ya uwepo wa imani zilizo simikwa katika anasa , zenye kuhamasisha ukosefu wa
uwajibikaji, usio ruhusu kujihukumu katika lolote, iwe kujirudi kimwili au katika
wito wa kiroho."Amesisitiza , uhuru wa kweli, huandamana na kutambua maana ya halisi
ya uhuru , kama tabia kuu ya ubinadamu.
Patriarca alihitimisha: "Pengine katika
muda huu wa ukimya na tafakari, kupitia ishara za unyenyekevu au ukali wa maisha
ya kila siku, tunaweza kufurahia kwa mara nyingine, maadili halisi na kujenga tena
mzunguko wa wema na maelewano, mshikamano na heshima na bila ubinafsi , kwa kuheshimiana
mmoja kwa mwingine. "