2012-11-30 16:17:38

Papa kufungua kipindi cha majilio akiwa na wasomi wa vyuo vikuu


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumamosi Mosi Desemba, majira ya jioni anakianza kipindi cha Majilio kwa sala ya masifu ya jioni , akiwa pamoja na wawakilishi kutoka Vyuo Vikuu vya "Roma Tre".
Ijumaa hii30 Septemba, Kardinali Antonio Maria Veglio, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kazi za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum, ameongoza Ibada ya Misa , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, hapa Vatican , ibada iliyohudhuriwa na umati wa wasanii wa Italia wajulikanao kama “ARTIGIANI”, wapatao elfu kumi,.
Wasanii hao wamekusanyika Roma kwa ajili ya kuadhimisha Siku Kuu yao mahalia pia kama maadhimisho ya mwaka wa imani , na mtazamo wa kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuazishwa shirika la Wahamiaji.
Wasanii hao wakiwa ni wanasarakasi, wachoraji picha barabarani , bendi na wanamuziki n.k, wana wanao kilisha familia kubwa ya wasanii, pia wametoa shuhuda wa imani, kupitia kazi zao za usanii barabarani na mitaani.

Wasanii hawa , pia majira ya saa za usiku, watafanya tamasha na muziki, katika uwanja wa Piazza della Popolo wa hapa mjini Roma.

Na Jumamosi asubuhi, pia wataandamana kisanii tokea Castel del'Angelo hadi Vatican , ambako watakutana na Papa katika ukumbi wa Paulo V1 majira ya saa tano za asubuhi.

Juhdi hizi zinaoongozwa na Kardinali Antonio Maria Veglio, kwa kushirikiana na Shirika la Wahamiajila Baraza laMaaskofu la Italia , na jimbo la Roma na Taasisi zingine mbalimbali .










All the contents on this site are copyrighted ©.