Maaskofu Katoliki wa New Zealand, wamewasilisha tamko lao kwa Kamati ya Kiserikali
, juu ya mswada unaotaka kubadilisha maana na neno ndoa.
Tamko la Maaskofu
limetaja imani yao kwamba, neno Ndoa, huonyesha kwa namna ya kipekee katika , uwajibikaji
wa kudumu wa kijamii, katika mahusiano kati ya mwanamme mmoja na mwanamke mmoja ,
mahusiano ambayo asili yake, huelekea katika kuumba uhai mapya wa binadamu.
Maaskofu
wanataka maana ya neno ndoa lilindwe kisheria, kwamba, asili ya ndoa ni muungano
kati ya mwanaume na mwanamke na si vinginevyo.
Katika hati yao wameeleza kwamba,
Kanisa Katoliki daima huhimiza ndoa ya mke na mme , kama ilivyo katiak asili yake
ya kuwa chimbuko na kituo msingi katika maisha ya kijamii, na pia hufanikisha mazingira
bora kwa ajili ya malezi ya kulisha familia na watoto. Na hivyo, utendaji wa wanandoa
ndiyo msingi wa taifa kuwa na jamii bora au taifa bora. Na hivyo Kanisa huunga
mkono taasisi na mafundisho yote yanayoandaliwa kwa ajili ya wake kwa waume wanaotarajia
kufunga ndoa ya mke na mme, ambamo hutolewa mada mbalimbali kama maandalizi kwao
ya kujenga familia bora, na pia kuelimishwa juu ya changamoto wanazo weza kupambana
nazo na jinsi ya kukabiliana na hali ngumu pale mmoja wao anapo fariki dunia au katika
hali za kutaka kutengana. Kanisa Katoliki linaweka bayana kwamba, huu si mjadala
juu ya ushoga, lakini ni swala la ufafanuzi juu ya asili ya neno ndoa, kwamba ni
mke na mme, ndoa inayo inadharirishwa na watu wa jinsia moja, wanaoishi pamoja,
na kutaka na kupata haki ya kutambulika kama wana ndoa. Kanisa Katoliki linarudia
tena kusisitiza kwamba asili ya ndoa inatokana na watu wawili mke na mme katika asili
ya tofauti zao kijinsia, kuungana pamoja kinyumba na kuuunda familia katiak muungano
wao. Kanisa Katoliki linatambua haki hii ya ndoa na hakuna binadamu anayeweza kuitangua.
Na kila binadamu ana haki ya kuingia katika muungano huu kwa uhuru kamili kama kutimiza
asili ya maumbile.