Wito wa Papa katika kuiadhimisha Siku ya Dunia dhidi ya Ukimwi.
Baba Mtakatifu, Jumatano hii amehimiza mashirika , taasisi na makampuni na watu wote
duniani , kufanya kila jitihada za kutokomeza virus vya ukimwi duniani. Papa alitoa
himizo Jumatano mchana wakati akihutubia mahujaji na wageni waliofika kusikiliza Katekesi
yake ya Jumatano hii.
Papa aliukumbusha umati huo kwamba, tarehe Mosi Desemba
ni Siku ya Dunia, inayoangalisha katika mapambano na maradhi ya Ukimwi, Maradhi yaliyoangamiza
maisha ya watu wengi, licha ya kuwa adha kubwa na mateso kwa watu duniani , hasa
kwa maskini na wanyoge zaidi duniani zaidi.
Na kwa namna ya pekee , Papa
alielekeza mawazo yake kwa watoto ambao kila mwaka, mpka sasa wanapata maambukizi
ya virusi kutoka kwa mama zao, licha ya uwepo uwezakano wa kuepusha na ambukizo hilo.
Katika kujali hilo, Papa ametoa ombi kwa mashirika na makampuni yote yanayoshughulika
na changamoto hii ya kupambana na virusi, na katika mazingira ya utume wa kanisa Katika
kazi ya zake kwa nyakati hizi, kufanikisha maisha ya furaha kamili kw afamilia kama
jukumu upendeleo kwa familia , ambamo ndani yake, maisha ya imani inawezekana kuliishi
kila siku kwa furaha, mazungumzo, kusameheana na kupendana. Papa amehimiza mipango
mingi hata katika utume wa Kanisa, kwa ajili ya kukuzwa juhudi zaidi , katika kutokomeza
janga hili.