Watanzania mlioko Diaspora jitokezeni kuchangia maoni kuhusu mustakabali wa Tanzania
kupitia Katiba
Dr. James A. Msekela, Balozi wa Tanzania nchini Italia anaendelea kuwahimiza watanzania
wanaoishi ughaibuni "diaspora" kujitokeza kwa wingi kuchangia maoni kuhusu mustakabali
wa Tanzania kupitia Katiba, zoezi linalotarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2014.
Dr. Msekela
anabainisha kwamba, Katiba ni Sheria Mama itakayokuwa na dhamana ya kuwaongoza Watanzania
kwa miaka ijayo, kumbe, hili ni zoezi nyeti linawawajibisha kujitokeza ili kutoa maoni
yao katika maeneo mbali mbali, lakini zaidi kuhusu uraia wa nchi mbili, kwani wao
ndio watu wanaoguswa zaidi na dhana hii.
Maeneo mengine tete ni kuhusu: Imani,
uhuru wa kuabudu na uhuru wa dhamiri; mambo yanayopaswa kuainishwa kikatiba.