Mkutano wa Kimataifa 1V juu ya Uwasilishaji Urithi wa Utamaduni.
Mkutano wa Kimataifa 1V juu ya mawasiliano katiak urithi wa utamaduni Kwa muda
wa siku tatu 5-7 Desemba 2012, katika jengo la Makumbusho la Vatican kutafanyika Mkutano
wa Kimataifa wa 1V, ukiongozwa na Mada: "Jinsi gani inawezekana kuwasilisha urithi
wa utamaduni katika jamii". Kongamano hili la siku tatu, litaziduliwa na Antonio
Paolucci, Mkurugenzi wa Majengo ya makubusho Vatican, pia atakuwepo Tullia Carettoni
Romagnoli , Mjumbe na Rais wa shirika la Italia la Makumbusho la Herity , pia atakuwepo
Kardinali Francesco Marchisano , Rais wa Tume ya Kimtaifa ya Herity. .................................................................................................................... Na
Jumanne 27 Novemba 2012, Kardinali Antonio Maria Veglia, alikutana na Wakurugenzi
wa Kitaifa kwa ajili a kazi za kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiolkuwa na makazimaalum
kw aajili ya ufunguzi wa kazi za mkutano , kama ilivyoadaliwa na Baraza la Mabaraza
ya Maaskofu ya Ulaya, utakao kamili tarehe 29 Novemba 2012. . Kardinali Veglio,
majira ya joni alizungumzia mada: "Mshikamano katika kazi za kichungaji kwa ajili
ya Uinjilshaji mpya". Na majira ya jioni , katika ujengo la Domus Maria , Mtaa wa
Aurelia 481, katika mazingira ya Mkutano huo, kulifanyika Ibada ya Misa . Kardinali
Antonio Maria Veglio , kwenye homilia yake , alionyesha kutambua haja ya kuwa na mbinu
ya kweli na ubinadamu, kuanzia ndani ya kanisa lenyewe , katika utaratibu wake wa
kuwapokea na kuwajali wahamiaji wanao “gonga" malangoni.
Alisema, hii inaonyesha
kwa namna ya pekee jinsi Upendo wa Kristu unavyotakiwa kutimizwa , kwa maneno mengine
ni “wito wa Kanisa kwa namna ya pekee kuwakarimu wahamaji na wenye shida , pia katika
mitazamo na mipango ya kichungaji na majadiliano , lakini pia kusaidia waaminifu
kuushinda moyo wa kujenga chuki na ubinafisi dhidi ya wageni wahamiaji.
Na
hivyo ,ameutaja mkutano huu kuwa ni somo linaonyesha mwelekeo katika tafakari halisi
za watu wanaohusika katika huduma ya kichungaji ya wahamiaji, kujenga ushrikiano
na umoja katika katika kuhudumia.
Na alimalizia kwa kuomba msaada wa Roho
Mtakatifu ili kwamba , ripoti ya wataalam, baada ya zoezi la kubadilishana mawazo
na uzoefu, iweze kutoa mapendekezo mapya, katika huduma ya kichungaji ya wahamiaji.
Na pia roho ya kukubali ushirikiano miongoni mwao, iweze kuelekeze katika mipango
ya maendeleo ya thabiti na mbinu mpya ya uinjilishaji.