2012-11-28 15:43:59

Kardinali Ravasi aridhia Tuzo ya Kardinali Michele Giordano


Kardinali Gianfranco Ravasi ameridhia kupokea tuzo ya Kardinali Michele Giordano ambayo hutolewa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni.

Mapendekezo ya kuchagua mshindi wa tuzo hii kwa namna ya pekee yamekuwa ya kuvutia, kutokana na waandaaji kufanikisha upigaji wa kura ya kumpata mshindi wa tuzo, kupitia ukurasa wa Facebook.

Udumishaji wa Tuzo hii ya Kardinali Michele Giordano, pia unahimizwa na Askofu Mkuu wa Napoli, Kardinali Crescezio Sepe Pia utoaji wa tuzo kwa Kardinali Ravas umeridhiwa na Mwenyekiti wa Tuzo hiyo, Fulvio Tessitore, na wajumbe wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni, kama kutambua uthabiti wa Kardinali Ravasi katika maamuzi yake.

Aidha imebanishwa kwamba, Kamati kwa ajili ya toleo la tuzo kwa mwaka 2013 imeundwa. Wajumbe wake wakiwa , Profesa Weaver, na kutoka kundi la waandishi wa habari kati yao ni Francesco Antonio Grana (Katibu wa Tuzo), Ottavio Lucarelli (La Repubblica, Rais wa Waandishi wa Habari katika kanda), Antonello Perillo (Rai), Marco Perillo (Corriere del Mezzogiorno), Alfonso Pirozzi (ANSA) na Petro Treccagnoli (Morning).

Mengi zaidi juu ya tuzo hii unaweza kuyapata katika ukurasa wa mtandao: www.libreriaorientaleditrice.it.

Na hapo Jumamosi Desemba 1 saa 12.30 katika Basilica la Capodimonte kutafanyika Ibada ya Misa katika kaburi la Kardinali Giordano, kwa ajili ya maadhimisho ya pili ya kifo chake.









All the contents on this site are copyrighted ©.