Kiko Urguello, mwanzilishi wa Ukatukumeni Mpya-atoa kitabu, jinsi alivyokutana na
Kristu .
Kardinali Antonio Cañizares, Mkuu wa shirika kwa ajili ya Ibada Takatifu , katika
utangulizi wa kitabu cha Kiko Uguello , Mwanzilishi wa njia ya Ukatukumeni Mpya "Neo-Catechumenal
Way , amesema, juhudi hizo ni zawadi ambayo Roho Mtakatifu amelipatia Kanisa lake
, kama njia ya majiundo mapya ya Mkristu, au kwa lugha nyingi mafundo mapya , na
kama chombo cha kuhamasisha na kukuza uinjilishaji mpya"
"Kardinali amemshukuru
Mungu kwa neema na maajabu makubwa yanayo endelea ndani ya Kanisa, kupitia njia
hii ya Neo, ambamo kwa neema na baraka za Kanisa : Mama Kanisa anashuhudia matunda
ya mabadiliko, ya maisha ya kikristo, na katika miito ya ukuhani na maisha yaliyowekwa
wakfu, na kazi za kimisionari za Kanisa, kama matunda ya upendo, na maisha katika
kutunza heri nane, ukarimu, na ya familia yenye maaisha ya kujifunua wazi, mmoja
kwa mwingine.
Na Kardinali Christoph Schönborn, askofu mkuu wa Vienna, ikichangia
maoni juu ya kuchapishwa kwa Kitabu cha Maisha ya Kiko Uguello, amekiita kitabu hicho
kuwa ni mwaliko katika uongofu binafsi. Na kwamba, Katekesi zilizo chapishwa katika
kitabu hiki zinavutia kwa sababu ya uwazi wake. Na hasa msisitizo kwamba , mimi
binafsi, bila ya uongofu binafsi, haiwezekani kuinjilisha. Na hivyo kwa anayetaka
kuinjilisha ni sharti ajiinjilishe yeye mwenyewe kwanza. Mlei mwanzilishi wa Jumuiya
ya Ukatukuemni mpya, "Neo Catechumenal Way", ametoa kitabu chake chenye maelezo binafsi
jinsi alivyokutana na Yesu Kristu.