Wakatoliki Wakoptic wa Misri, kutazama mbinu za pamoja kukabiliana na upinzani.
Jumanne ya wiki hii, Ujumbe wa Kanisa Katoliki la Kikoptic nchini Misri , unatazamia
kukutana na Patriaki Tawadros, Papa mpya wa Kanisa la kikoputic la Kiotodos aliyesimikwa
rasmi, Jumapili ya tarehe 18 Novemba 2012. Kwa mujibu wa Askofu Kyrillos William
wa Assiust , ambaye pia ni Vika katika Upatriaki Katoliki wa Kikoptic, wa Misri,
lengo la ziara ni kupata muda wa kushauriana jinsi wanavyoweza kuratibu kwa vizuri
zaidi shughuli, za kanisa kwa nyakati hizi ambamo taifa la Misri linakabiliwa na
machafuko ya kisiasa. Vurugu za upinzani na ghasia zilizoibuka , ambamo wapinzani
wanataka uwezo wa Rais upunguzwe. Kama ilivyokuwa wakati wa upinzani dhidi ya
Rais Hosni Mbaraka , pia wakati huu wapinzani wamejazana katika uwanja wa Taharir,
Cairo kudai demokrasia zaidi . Na Mashabiki wa Rais Morsi wanadai kwamba, kwa wakati
huu ni muhimu Rais kuwa na uwezo zaidi, kwa ajili ya udumishaji wa mabadiliko ya
kidemokrasia. Madai yanayotajwa na wapinzani kwamba , ni mwelekeo unaoongoza katika
mfumo wa kidikteta, na kwamba Rais Morsi anataka kuwa Pharao Mpya. Wiki iliyopita,
wawakilishi wa jumuiya za Kikristu walijiondoa katika Baraza la Kikatiba, kama jibu
kwa shinikizo linalotaka mabadiliko kwa mujibu wa makubaliano ya kikatiba. Na
Daima senti ya mjane maskini ni nguvu ya tumaini jipya – Burkina Faso. Askofu
Prosper Kontiebo , wa Jimbo Jipya Katoliki la Tenkodogo , Kusini mwa Mji wa Ouagadougou,
Burkina Faso, ambaye amekuwa ni Askofu wa 400 katika historia ya shirika la Camellius,
waliofika kwa mara ya kwanza , Oaugadougou, mwaka 1966, hivi karibuni, ameshuhudia
jinsi senti ya mjane ilivyo na nguvu ya kumpa mtu tumaini jipya. Ushuhuda huo umeelezwa
hivi karibuni na Padre Felice Rufini wa shirika la Wakamillioni, kwa shirika la
Fides . Askofu Kontiebo, aliishuhudia nguvu ya senti ya mjane, akirejea Injili
ya Kristu, iliyosomwa Jumapili ya 32 ya mwaka , ambamo Yesu aliwatazama waliokuwa
wakitoa sadaka , matajiri wakitoa kiasi kikubwa na mwanamke mjane kutoa senti mbili
alizokuwa nazo (MK 12:41-44). Askofu anasema , senti hizo mbili, ni tumaini jipya
alilopata pia, wakati alipo mtembelea bibi yake mkongwe, kwa nia ya kuaga kwamba,
atakwenda Roma kukutana na Papa. Bibi huyo mkongwe baada ya kusikia mjukuu wake
anakwenda Roma kuonana na Papa, aliona ni nafasi pia kwake ya kutoa mchango wake
kwa kazi za Papa, mara alinyanyuka na kuvuta kisanduku chake na kumpa kiasi cha franc
250 ambazo ni sawa na senti 38 za Euro, akisema, fedha hiyo ni mchango wake kwa
Papa. Asema," kiasi hiki kidogo ninachokupa si chako, ila utakapofika katika Kanisa
Kuu la Mtakatifu Petro, ziweke katika kisanduku kilicho chini ya miguu yake Petro
, kwa ajili ya Papa ". Askofu anasema, mchango mdogo wa bibi huyu, unapaswa kumgusakila
muumini wa kanisa katika nyakati hizi zetu, ambamo Kanisa linapambana na changamoto
nyingi , lakini daima linamulikiwa na neema ya mwanga mkuu wa tumaini.