2012-11-26 15:27:18

Vyombo vya habari vyatakiwa kutoa taarifa za kweli DRC.


Askofu Bernard Kasanda wa Jimbo ka Mbuji Mayi, amelaani vikali ghasia za mapigano zinazoendeshwa Mashariki mwa Congo na kukosekana kwa habari za kina na kweli katika vyombo vya habari, juu ya ghasia hizo.

Askofu Bernard ameeleza hilo wakati akizungumza na shirika la Msaada katika Kanisa Hitaji, wakati akizungumzia hali halisi katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo , na uwezo wa jumuiya ya Kimataifa katika kukabiliana na machafuko yanayoendelea kaskazini mwa Kivu.

Askofu Bernard ameliambia shirika hili la Kipapa kwamba hawakutazamia machafuko hayo kuibuka kwa kasi namna hiyo katika eneo la Goma. Na Hii haina maana kufuta kile kilichotokea katika miaka michache iliyopita, na jumuiya ya Umoja wa Mataifa kula njama kwa , kuichagua Rwanda kama mjumbe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , licha ya Rwanda kushutumiwa kukiuka mshikamano wa kimataifa, katika eneo la Kongo, iambako inaonekana wazi Rwanda kuendeleza uvamizi Mashariki mwa sehemu ya Congo.

Na kwamba, utajiri mkubwa wa madini na uwepo wa mafuta ni miongoni mwa sababu kubwa za kuyumba kwa eneo hilo. Askofu anaamini kwamba "kama hakuna juhudi za kukomesha maasi hayo kwa haraka, waasi hao wataendela na masahmbulizi hadi Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Kasanda, tumaini la utendaji wa Tume ya kulinda amani ya umoja wa Mataifa kwa kazi yake ya miaka kumi na minne , inaonekana kutokuwa na maana yoyote. “Walinzi wa amani wa kisiasa na mamlaka ya Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiwataka watu watulie na wasiogope maana hakuna cha kuwaumiza, lakini sasa waasi wamelishika eneo hilo la mashariki ya nchi, bila ya kuguswa".

Askofu Bernard, ametoa wito kwa vyombo vya habari kutoa taarifa za kweli na si habari potofu. Kwa taarifa za sasa hakuna anaelewa uzito wa kile kinachotokea dhidi ya utu wa binadamu, unaofinyangwa finyangwa huko Kongo, na kusababisha watu kurudi katika dimbwi la aibu na unyonge ".










All the contents on this site are copyrighted ©.