2012-11-26 15:42:34

Papa akutana na Makardinali wapya sita wakiwa na familia zao


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumatatu hii nyakati za mchana alikutana na Makardinali wapya wakiwa wameandamana na familia zao.
Katika hotuba yake , alionyesha mwendelezo wa furaha yake ya tangu Jumamosi , alipowasimika Makardinali wapya sita, na kwamba muda wote amekuwa akitolea sala zake kwa ajili ya muungano thabiti , kama ilivyokuwa katika siku hizi , ambamo Kanisa la ulimwengu , tena kwa mara ingine , katika mkusanyiko huo,wameuishi ushuhuda wa kanisa zima la Ulimwengu, likionyesha ishara ya matumaini kwa watu wote.

Papa aliendelea kuonyesha furaha ya kuwapokea kwa mara ingine na kuwakaribisha katika hali ya kawaida kama familia moja. Na kupitia kwa makardinali wapya, Papa aliomba wafikishe salam zake kwa ndugu zao, marafiki na wale wanaowasindikiza , kwa nia kushuhudia tukio hili makini na muhimu.

Papa alirudia kuwataja Makardinali wapya aliwoasimika Jumamosi: Kardinali James Michael Harvey, Padre Mkuu wa Kanisa Kuu la Kipapa ya Mtakatifu Paulo Nje Kuta. Kardinali Baselios Cleemis THOTTUNKAL, Meja Askofu Mkuu wa Trivandrum ya Syro-Malankaras (India), Kardinali John Olorunfemi ONAIYEKAN, Askofu Mkuu wa Abuja (Nigeria), na Kardinali Luis Antonio Tagle, Askofu Mkuu wa Manila (Ufilipino). Pia azikaribisha familia na marafiki, na waamini wote ambao walioongoza na Makardinali.

Hotuba yake ilitoa ufufnuzi mfupi juu ya asili ya Chuo cha Makardinali, kwamba asili yake inahusiana na Makleri wa kale wa Kanisa la Roma, waliotakiwa kumchagua Khalifa wa Petro na kushauriana naye katika masuala muhimu ya Kanisa. Iwe kwa ajili ya kazi za Idara za Kanisa zinazojulikana kama ofisi ya Curia ya Roma, au katika huduma zake kwa Makanisa dunia kote. Makardinali kwa namna ya pekee , wanal jukumu kwa namna ya pekee , kushirikiana na Papa , kwa ajili ya kufanikisha kazi za Papa kwa Kanisa zima la ulimwengu.

Papa aliendelea kufafanua maana ya rangi nyekundu ya za mavazi yao, akisema, ni mapokea ya kitamaduni yanayoonyesha dhahiri , ishara ya kukubali kuwajibika kwa uthabiti katika kutetea kundi la Kristo hata kwa kumwaga damu yao. Papa alionyesha imani yake kwamba, wakati Makadinali wapya wanaanza utume wao mpya , wataimarishwa na msaada wa sala za waumini na kwa kushikamana na Askofu wa Roma, kwa ajili ya kukuza utakatifu dunian, ushirika na amani ya Kanisa.

Papa alimalizia hotuba yake kwa kuwatakia Makardinali kila lililo jema katika kazi yao mpya na kwa kuwa washarika katika Chuo cha Makardinali! Huduma yao na iimarishwe na ahadi mpya za kumsaidiana na Khalifa wa Petro, katika huduma yake nzima ya Kanisa. Na waendelee na ujasiri na nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu, mwenye uwezo wa kuwaimairisha na kuwaunganisha na upendo wa Kristu na Kanisa lake. Kwao wote aliwaweka chini ya ulinzi wa Mama wa Mungu Bikira Maria, Mama wa Mitume na kuwapa baraka zake za Kitume.







All the contents on this site are copyrighted ©.