2012-11-26 09:32:00

Papa ahimiza mwendelezo wa Kazi za kumkomboa binadamu dhidi ya dhambi


Jumapili iliyopita, baada ya Ibada ya Maadhimisho ya Siku Kuu ya Kristu Mfalme, Baba Mtakatifu alisala sala ya Malaika wa Bwana, mbele ya maelfu ya mahujaji na wageni walio kusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican. Katika umati huo, pia walikuwepo Makardinali wapya sita aliowasimika katika daraja la Ukardinali siku ya Jumamosi.
Hotuba ya Papa ya wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, ilihimiza Waamini kuendeleza kazi ya Mungu ya kumkomboa binadamu dhidi ya dhambi, wakianza na wao wenyewe, kuiongokea Injili ya Kristu na kutembea katika nyanyo za Kristu Mfalme , aliyekuja si kutumikiwa bali kutumikia na kutoa shuhuda za kweli ulimwenguni.
Alisema kwamba , leo Kanisa linaadhimisha Siku Kuu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Mfalme wa Ulimwengu. Siku Kuu hii inakuja mwisho wa mwaka kiliturujia na inajumuisha fumbo takatifu la Yesu "mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu na mtawala wa mamlaka yote ya dunia" , mwenye kuelekeza nadharia zetu zote katika utambuzi kamili wa Ufalme wa Mungu, wakati Mungu atakuwa yote kwa vyote. " (taz. 1Kor 15:28.).
Papa alieleze hilo na kutazamisha kwa maelezo yake kwa Mtakatifu Cyril wa Yerusalemu aliyesema: "Sisi hatutangazi tu ujio wa kwanza wa Kristu lakini pia kuja kwake mara ya pili ambalo ni jambo la kuvutia zaidi kuliko hata la kwanza. Katika ukweli wake , ujio wake wa kwanza, alidharirishwa kwa mateso, lakini ujio wa pili itakuwa ni taji na kilemba cha Utukufu wa Kimungu ...Katika ujio wake wa kwanza , alidharirishwa msalabani , lakini katika uji wa pili atazungukwa na kutukuzwa na umati wa malaika.
Papa anasema, Ujumbe wote wa Yesu na maudhui ya ujumbe wake ni kuutangaza Ufalme wa Mbinguni na aliouanzisha miongoni mwa watu, kwa ishara na maajabu. Na kama Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, unavyotukumbusha , zaidi ya yote, "Ufalme huo, unaonekana kwanza kupitia ubinadamu wa Kristu " ("Lumen gentium," 5), kupitia njia ya kifo chake msalabani na ufufuko wake , ambamo alidhihirishwa kuwa ndiye Bwana wa milele, Masiya na kuhani. Ufalme huo wa Kristo, ulidhaminishwa kwa Kanisa , kama "mbegu" na "mwanzo" wa kazi ya kutangaza na kueneza kwa watu wa mataifa yote, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu . Wakati wa mwisho wa nyakati , Bwana atauwasilisha ufalme wa Mungu Baba , na ataonekana kwa wale wote ambao walioishi kwa mujibu wa amri yake ya upendo.

Papa alieleza na kuongeza kwamba, “ sisi sote tumeitwa kuiendeleza kazi hii ya Ukombozi wa Mungu, tukianza na sisi wenyewe kukubali kubadlishwa na Injili na kuwa imara katika kuifuta njia ya Mfalme ambaye hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kutoa ushuhuda kwa ukweli (taz. Marko 10:45 ; Yohana 18:37)”.
Kwa maelezo hayo, Papa alitoa mwaliko kwa kila mmoja kuwaombea Makardinali wapya aliowasimika siku ya Jumamosi , ili Roho Mtakatifu awaimarishe katika imani na katika upendo , akiwajaza pia na zawadi ya baraka na neema nyingi , ili waweze kuuishi wajibu wao mpya kama ahadi zaidi kwa Kristo na Ufalme wake. Papa aliongeza, Makardinali hawa wapya katika Chuo cha Makardinali, wanawasilisha vyema mtazamo mpana wa Kanisa la Ulimwengu wakiwa ni wachungaji wa Makanisa, nchini Lebanoni, India, Nigeria, Colombia na Ufilipino na mmoja wao amekuwa katika utumishi wa Jimbo Takatifu kwa miaka mingi. .

Papa aliomba msaada na ulinzi wa Maria Mtakatifu Sana kwa kila mmoja wao na kwa ajili ya uaminifu wa huduma mpya waliyokabidhiwa. Bikira Maria na atusaidie sote kuziishi nyakati hizi za kusubiri kurudi kwa Bwana, tukitolea sala kwa roho moja : "Ufalme wako uje," na wakati tunafanya utume wa kufikisha kazi za mwanga wa Injili , unaotuweka karibu zaidi na Mbingu , katika utambuzi kwamba, kupitia sulubu za kihistoria , Mungu anaendelea kuujenga Ufalme wake wa Upendo.

Baba Mtakatifu, baada ya sala ya Malaika wa Bwana , alisalimia katika lugha mbalimbali. Akitoa slaam hizo kwa lugha ya Kispanishi, alilikumbuka tukio la Maria Troncatti, Mtawa wa kike wa wa Shirika la Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo, aliyetangazwa kuwa Mwenye Heri siku ya Jumamosi. . Mwenye Heri Maria Troncatti, alizaliwa Val Camonica, Italia na alikuwa muuguzi wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia. Baadaye alikwenda Ecuador ambako kwa hiari yake aliamua kuyaishi maisha yaliyowekwa wakfu kwa ajili ya kuwahudumia watu fukara katika misitu ya Ecuador, akiindeleza kazi ya uinjilishaji na ustawi wa ubinadamu. Papa alimshukur u Mungu kwa ajili ya ushuhuda na ukarimu wa Mwenye Heri huyo







All the contents on this site are copyrighted ©.