2012-11-26 09:17:22

Makardinali Wapya wapangiwa Makanisa ya huduma mjini Roma


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumamosi tarehe 24 Novemba 2012, baada ya kuwasimika rasmi Makardinali wapya, aliwagawia pia Makanisa ambamo watayatumia kwa ajili ya kutoa huduma ya kichungaji hapa mjini Roma.
Kardinali James Michael Harvey: atatoa huduma kwenye Kanisa la San Pio V kule Villa Carpegna.
Kardinali Bechara Boutros Rai O.M.M.
Kardinal Baselios Cleemis Thottunkal, atakuwa mhudumu wa Kanisa la San Gregorio VII.
Kardinal John Olorunfemi Onaiyekan, atakuwa mhudumu wa Kanisa la San Saturnino.
Kardinal Ruben Salazar Gomez, atakuwa mhudumu wa Kanisa laSan Gerardo Maiella.
Kardinal Luis Antonio G. Tagle, atakuwa mhudumu wa Kanisa la San Felice da Cantalice a Centocelle.








All the contents on this site are copyrighted ©.