2012-11-24 13:55:29

Wawakilishi wa Makardinali Wapya!


Ibada ya kusimikwa kwa Makardinali wapya sita, iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumamosi tarehe 23 Novemba 2012, imehudhuriwa na wawakilishi maalum kutoka Lebanon, ujumbe ambao umeongozwa na Jenerali Michel Sleiman, Rais wa Lebanon. Kutoka nchini Ufilippini, ujumbe umeongozwa na Bwana Jejomar C. Binay, Makamu wa Rais wa Ufilippini.

Ujumbe wa waamini na watu wenye mapenzi mema kutoka India, umeongozwa na Profesa P. J. Kurien, Rais wa Bunge la India. Kwa upande wa Kardinali John Onayeikan, ujumbe kutoka Nigeria uliongozwa na Seneta David Mark.

Licha ya kuhudhuria Ibada ya kusimikwa kwa Makardinali wapya, wawakilishi hawa pia watashiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, Maadhimisho ya Sherehe ya Kristo Mfalme, ambayo Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita pamoja na Makardinali hawa wapya wataongoza Ibada ya Misa Takatifu.







All the contents on this site are copyrighted ©.