2012-11-23 10:10:08

Siku ya Kimataifa ya kufuta manyanyaso kwa wanawake


Tarehe 25 Novemba ni Siku ya Kimataifa ya kufuta madhulumu na manyanayso kwa wanawake.

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki Moon, kwa ajili hii, unataja mamilioni ya wanawake na wasichana kote duniani hupambana na uovu wa kushambuliwa, kubakwa na hata kuuawa, licha ya haki kunyimwa haki msingi za binadamu. Hayo hufanyika tangu mazingira ya ndani majumbani , mitaani, mashuleni, kazini na katika jamii zao. Karibia asilimia 70% ya wanawake wana uzoefu wa mateso ya kimwili au ukatili wa kijinsia katika maisha yao. Aidha karbia robo ya wanawake wajawazito wameathirika kwa manyanyaso .ya wanaume.

Mara nyingi wahusika hubaki bila kuadhibu, kutoka na wanawake na wasichana, kushindwa kupta ujasiri wa kueleza waziwazi yanayo wasibu kutokana na uwepo wa utamaduni wa kutokujali malalamiko yao na hofu za kudhulumika zaidi iwapo watatoa ukweli wa manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa wenzi wao wanaume.

Kwa hiyo ni muhimu wanawake, kupata ujasiri wa kupambana na hisia ya hofu na aibu, na kueleza ukweli pale wanapoteswa au kudhulumiwa na wanaume, na kukabiliana na uhalifu huu unyanyapaaji wa kijamii. Inapaswa wahusika wa ghasia hizo kuona aibu kwa matendo yao maovu.

Ujumbe wa Katibu Mkuu Ban Ki Moon, unaendela kuhimiza wake kwa waume, kujenga umoja na mshikamano imara, kwa ajili ya kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa kushirikiana na serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla.

Ameendelea kukumbusha kwamba, mwaka jana, kupitia juhudi hizi za kukomesha manyanayso dhidi ya wanawake, alitoa ombi kwa vijana wote duniani , kwa namna ya pekee kutoa mchango wao , kwa sababu hii. Na ameonyesha kuridhika kwamba vijana wengi wameitikia wito huo wa kusitisha ujinga wa kutovumilia wengine na mitazamo mingine hasi, kwa kuwa kumekuwa na maombi mengi yanayoongeza sauti ya Umoja wa Mataifa katika lengo la kukuza haki za binadamu na kujiunga na vikosi vya kutoa msaada kwa waathirika.

Na kwamba , Umoja wa Mataifa unalifanyia kazi hili, kupitia kampeni za kujenga ufahamu bora zaidi, kupitia mipango ya elimu ya umma.

Katibu Mkuu anaendelea kubaini kwamba, mwezi huu, Umoja wa Mataifa, kupitia Mfuko wa Fedha kwa ajili ya Kukomesha Unyanyasaji dhidi ya Wanawake, umetangaza mipango ya kutenga dola milioni nane kwa ajili ya mipango ya ndani katika nchi nane.

Na pia kumeenekana juhudi zaidi katika mtandao wake unaouuganisha viongozi wanaume , kwa lengo la kupanua hatua za utendaji katika kukabiliana na tatizo hili kupitia kampeni za kukusanya maoni ya umma na uboreshaji wa sheria na uwajibikaji wa serikali mahalia. Hata hivyo ameonya , juhudi hizi, bado maendeleo yake yanapambana na changamoto ya utamaduni wa ubaguzi, unaendeleza vurugu na manyanyaso.

Hivyo katika Maadhimisho ya Siku hii ya kufuta manyanyaso kwa wanawake, Katibu Mkuu ametoa wito kwa serikali zote, kuweka ahadi, ya kukomesha aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote, na anamsihi kila mtu kusaidia ufanikishaji wa lengo hili muhimu.








All the contents on this site are copyrighted ©.