2012-11-23 14:49:14

Rais Michel Sleiman wa Lebanon akutana na Benedikto XVI mjini Roma


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Ijumaa, amekutana na kuzungumza na Rais Michel Sleiman wa Lebanon, nchi ambayo Baba Mtakatifu aliitumia kuwasilisha matunda ya Sinodi ya Maaskofu Katoliki Mashariki ya Kati, Mwezi Septemba 2012.

Rais Sleiman amemshukuru Baba Mtakatifu kwa kumteua Patriaki Bechara Boutros Rais wa Kanisa la Kimaroniti kuwa Kardinali. Kardinali mteule Bechara Boutros Rais anasindikizwa na jumla ya waamini 500 kutoka Lebanon ambao wamekuja kushuhudia tukio hili la kihistoria.







All the contents on this site are copyrighted ©.