Maaskofu Marekani wachangia fedha kwa ajili ya mikakati ya shughuli za kichungaji
Amerika ya Kusini; kielelezo cha mshikamano wa upendo na kidugu
Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani katika mkutano wao uliohitimishwa hivi karibuni
wamepitisha jumla ya miradi mia moja na sitini, yenye thamani ya dolla za kimarekani
zipatazo millioni 2.3, itakayotolewa kwa ajili kugharimia miradi ya shughuli za kichungaji
inayofanywa na Kanisa Amerika ya Kusini.
Hiki ni kielelezo cha mshikamano
wa upendo, kwa Kanisa Amerika ya Kusini ambalo kwa siku za hivi karibuni limetikiswa
na majanga asilia yaliyosababisha maafa na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.
Fedha
hii ya msaada itatumika kugharimia miradi iliyokoHaiti, Chile na Cuba. Lengo ni kusaidia
ujenzi wa miundombinu ya Makanisa yaliyoharibiwa hivi karibuni na tufani ya Sandy
pamoja na miradi mingine inayopania kuimarisha shughuli za: majiundo ya viongozi wa
Kanisa pamoja na nchi ambazo zitashiriki katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani
kwa mwaka 2013, itakayofanyika nchini Brazil.