2012-11-17 08:45:35

Mikakati ya CUEA katika mchakato wa Uinjilishaji Mpya Chuoni hapo!


Monsinyo Pius Rutechura, Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki na Kati, CUEA katika mahojiano na Radio Vatican anabainisha umuhimu wa Uinjilishaji Mpya unaondeshwa CUEA kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka wa Imani, uliozinduliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita. RealAudioMP3

Dhamana hii inatekelezwa kwa namna ya pekee kwa njia ya utume wa maisha ya kiroho kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu pamoja na kuendelea kuimarisha vyama vya kitume ambavyo ni msaada mkubwa katika maisha ya kiroho kwa wanafunzi.

CUEA inaendelea kujiimarisha ili kuhakikisha kuwa inawajengea wanachuo wake uwezo wa kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya kumtumikia Mungu na jirani sanjari na ujenzi wa misingi ya maadili na utu wema, changamoto endelevu katika Jamii nyingi Barani Afrika. Mpango huu unakwenda sanjari na uwezeshwaji wa viongozi wa Kanisa na kwa namna ya pekee, viongozi wa utume wa vijana, ili waweze kutoa ushauri makini kwa vijana katika shida na mahangaiko yao ya ndani.







All the contents on this site are copyrighted ©.