2012-11-14 15:22:44

Monsinyo Josè Avelino Bettencourt ateuliwa kuwa Kiongozi Mwandamizi wa Itifaki mjini Vatican


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Monsinyo Josè Avelino Bettencourt, kuwa Kiongozi Mwandamizi wa Itifaki mjini Vatican. Kabla ya uteuzi wake alikuwa ni mshauri wa Balozi za Vatican. Alizaliwa tarehe 23 Machi 1962 mjini Azzorre, Ureno.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, alipadrishwa tarehe 23 Juni 1993 kwa ajili ya Jimbo kuu la Ottawa, Canada. Alianza kutoa huduma za kichungaji mjini Vatican hapo tarehe Mosi, Julai 1999. Amewahi kutekeleza majukumu na utume wake kwenye Balozi za Vatican nchini DRC na baadaye alijereshwa tena mjini Vatican kuendelea na utume wake katika kitengo cha mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.