2012-11-14 09:23:15

Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, Rio de Janeiro, 2013


Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani itakayofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Julai 2013, huko Rio de Janeiro, imebainisha kwamba, Serikali ya Brazil, imesema kwamba, kwa mahujaji wote watakaoshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa hawatalazimika kupata hati ya kuingilia nchini humo.

Ili kufanikisha dhamana hii, mahujaji watalazimika kujaza fomu maalum inayotolewa na Wizara ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa; watatakiwa kuwa na hati za kusafiria pamoja na hati ya utambulisho kutoka Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa mwaka 2013.

Mahujaji watakaoshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani wanaruhusiwa kuendelea kwenda mjini Rio de Janeiro hadi tarehe 28 Julai 2013. Hati ya kusafiria itadumu kwa siku tisini. Na wale ambao watakuwa wamechaguliwa kwa kazi ya kujitolea wanaweza kuishi nchini Brazil kwa kipindi cha mwaka mmoja.







All the contents on this site are copyrighted ©.