2012-11-13 08:47:30

Papa ateuwa viongozi wa Taasisi Mpya ya Lugha ya Kilatini


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Profesa Ivano Dionigi kuwa Rais wa Taasisi ya Lugha ya Kilatini. Wakati huo huo, Mheshimiwa Padre Roberto Spataro ameteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Taasisi hii inayopania kukuza na kuendeleza lugha ya Kilatini ndani ya Kanisa.

Uteuzi wao utadumu katika kipindi cha miaka mitano. Taasisi hii itakuwa ni jumla ya wakufunzi na wasomi wasiopungua hamsini, watakaoteuliwa na Katibu mkuu wa Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.