2012-11-12 15:09:22

Monsinyo Fortunatus Nwachukwu ateuliwa kuwa ni Balozi Mpya wa Vatican nchini Nicaragua


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Monsinyo Fortunatus Nwachukwu kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Nicaragua pamoja na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa ni Afisa Mwandamizi wa Itifaki mjini Vatican.

Askofu mkuu mteule Fortunatus alizaliwa Ntigha, Nigeria kunako tarehe 10 Mei 1960. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 17 Juni 1984. Alianza kutoa huduma za kitume mjini Vatican tarehe Mosi Julai 1994. Amewahi kufanya kazi katika Balozi za Vatican nchini Ghana, Paraguay, Aligeria na kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zenye makao yake mjini Geneva.

Kunako tarehe 4 Septemba 2007, aliteuliwa kuwa ni Afisa Mwandamizi wa Protakali mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.