2012-11-09 08:19:00

Marehemu Askofu Balina mtu wa watu na chachu ya maendeleo apumzike kwa amani!


Monsinyo Pius Rutechura, Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki na Kati, CUEA anasema wameupokea msiba wa Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki Shinyanga anayezikwa Jumamosi tarehe 10 Novemba 2012 kwa mshtuko, imani na matumaini katika maisha ya uzima wa milele. RealAudioMP3

Binafsi alimfamu Askofu Balina kwa karibu zaidi alipokuwa Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye alipokuwa Katibu mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA. Kwa hakika, alikuwa ni mtu wa watu, mchangamfu na aliyewajali wote bila ubaguzi. Alikuwa na kipaji cha ugunduzi na daima aliibuka na mawzo na changamoto mpya zilizopania kumletea mtanzania maendeleo endelevu: kiroho na kimwili.

Alitamani kuona kwamba, Kanisa linakuwa mstari wa mbele katika huduma kwa kuzingatia misingi, maadili na Mapokeo ya Kanisa, ili liweze kujitegemea kwa raslimali watu walioandaliwa barabara, tayari kuchakarika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao. Matunda yanaonekana katika Sekta ya Afya.







All the contents on this site are copyrighted ©.