Unganisheni nguvu kuokoa maisha ya watoto chini ya miaka 5 wanaofariki dunia kutokana
na baa la njaa Kusini mwa Jangwa la Sahara
Baa la njaa Barani Afrika linaendelea kuwa ni chanzo kikuu cha vifo vya watoto wengi
wenye umri chini ya miaka mitano, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hii ni kutokana na
uwepo wa utapiamlo wa kutisha unaosababishwa kwa namna ya pekee na: ukame wa muda
mrefu pamoja na mfumuko wa bei za mazao ya chakula. Ukosefu wa chakula na lishe bora
kwa watoto wenye umri wa miaka mitano, umepelekea watoto hawa kudumaa na matokeo yake
ni kushindwa pia katika masomo.
Taarifa hii imetolewa hivi karibuni wakati
wa maadhimisho ya Siku ya Lishe na Usalama wa Chakula Barani Afrika. Katika maadhimisho
haya, wadau mbali mbali waliziomba Serikali, wahisani na vyama vya kiraia kuunga mkono
juhudi za kupambana na baa la njaa Barani Afrika, kama njia ya kuokoa maisha ya watoto
wenye umri chini ya miaka mitano.