2012-11-05 15:06:11

katika Amri ya Upendo mna mawili yasiyotengana-Papa


Jumapili iliyopita, Baba Mtakatifu Benedikto XV1, alihutubia makumi ya maelfu ya mahujaji na wageni , katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Mahubiri yake ililenga katika Somo la Injili juu ya Amri kuu iliyotajwa na Yesu, Amri ya Upendo.
Papa alibainisha kwamba, Amri kuu iliyofundishwa na Yesu, mna mawili yasiyo tengana, upendo kwa Mungu na jirani.
Papa aliendeela kutafakari amri ya upendo akiangalisha pia katika maisha ya Watakatifu ambao Mama Kanisa ameadhimisha kumbukumbu yao hivi karibuni , wote katika ujumla wao na pia kama mmojammoja. Alisema maisha yao yanadhihirisha , manufaa ya kuuishi uaminifu wa neema za Mungu na jitihada za kuizingatia amri ya upendo. Katika ukweli, ni kuzamisha mahusiano ya kina na Mungu , kama jinsi mtoto anavyokuwa na mahusiano mazuri na wazazi wake , mama na baba, na ndivyo ilivyo kwa anayeiishi amri ya Upendo kikamilifu.
Papa alimtaja kama mfano, Mtakatifu Yohane wa Avila , ambaye hivi karibuni alimtagaza kuwa mwalimu wa kanisa , kwamba, hati zake za mwanzo juu ya upendo wa Mungu, alitaja sababu zinazo sukuma mioyo yetu katika upendo wa Mungu, kwamba ni upendo wa kina wa Mungu, usiotafuta kunufaika, bali ni majitolea ya ndani yasiyotafuta faida. Ni upendo thabiti usiyosaza kitu katika majitoleo ya kisadaka. Na kwamba, licha ya kuwa amri , upendo ni zawadi , zawadi halisi ambayo Mungu anaturuhusu sisi binadamu kuifahamu na kuiishi , ili kama ilivyo mbegu, ikipandwa, huota,kuchanua na kukua.

Papa aliendela kufundisha kwamba, kama upendo wa Mungu umepandikiza mizizi yake kwa kina ndani ya moyo wa binadamu , hapo mtu huyo huweza kuwapenda hata wale ambao hawastahili , kama Mungu pia anavyotupenda sisi. Baba na Mama hawapendi watoto wao, si tu kwa sababu wanastahili kupendwa , lakini ni wajibu wa maisha , ikiwemo kuwaelimisha pale wanapofanya makosa .
Na kutoka kwa Mungu tunajifunza kupenda mambo mazuri na kamwe ubaya. Tunajifunza kusaidiana mmoja kwa mwingine, si katika mtazamo wa Macho ya kibinadamu , lakini kwa macho ya Kimungu , kuitazama sana sura ya Yesu Kristu, aneno aliyemwilishwa na kukaa nasi. Mtazamo uliojikita ndani moyo, na kutokeza hadi nje , ukienda zaidi ya kuonekana , na kunasa kwa kina hamu ya kujaliana mmoja kwa mwingine.
Kusikilizwa na kusaidiwa, kwa Upendo. Na kinyume chake pia, kuwa tayari kujifunua kwa mwingine , kama Kristu ,alivyojitolea sadaka , nasi pia tunapasw3a kuonekana na kusema mimi pia ninajifunua katika hamu ya kutaka kumjua Mungu kujisikia kwamba Yupo na ndiye Uzuri. Upendo wa Mungu na Upendo kwa jirani usioweza kutenganishwa katika mahusiano ya mmoja kwa mwingine. Yesu Kristo hakulibuni hili lakini alildhirisha ndivyo ilivyo, kuwa ni amri kuu pekee. Na hakufanya hivyo kwa maneno tu lakini kwa ushuhuda wa umwilisho wake katika fumbo la wokovu, lililofumbatwa ndani ya upendo wa Mungu na jirani, kama ilivyo mikono ya msalaba, mmoja wima na mwingine mstatili. ukiomdpa mmoja unakuwa si tena msalaba.
Ni katika Fumbo la Ekaristi Takatifu, tunamo pata zawadi hii ya upendo , zawadi ya majitoleo yake mwenyewe , ya kuwa mkate wa upendo, ili pia sisi tupendane sisi kwa sisi kama yeye anavyotupenda.
Papa alimalizia kwa kuomba msaada wa Bikira Maria, ili kila Mkristo aweza kutambua jinsi ya kuionyesha imani yake kwa Mungu wa Kweli Mmoja, kupitia shuhuda za maisha ya upendo kwa jirani.








All the contents on this site are copyrighted ©.