2012-11-03 14:50:06

Tahariri na Philomeno Lopez


Kazi tuliyo jipangia wenyewe kwa ajili ya tahariri hii, ni kutengeneza orodha ya masuala muhimu yatakayo sindikiza Maaskofu wa Afrika katika utume wa Kanisa wakati wa Sinodi , juu ya uinjilishaji mpya. Na majibu tuliyoyapata kutoka kwa wengi tuliozungumza nao ni, "Tumekuja kusikiliza, na hivyo ni muhimu kwanza kusikiliza "


Kwa mtazamo huo wengi waliomba kuahirisha kwanza mahojiano hadi siku za baadaye, na pengine labda karibu na mwisho wa Sinodi, ili waweza kufanya tathimini ya matazamio ya sinodi na mchango unaoweza kutolewa na Afrika katika kukabiliana na changamoto za uinjilishaji mpya .


Maaskofu wote walio hojiwa walionekana kuwa na jibu linalofanana, Kanisa Afrika kwa wakati huu, liko zaidi katika harakati za kutafuta njia zinazofaa, kutekeleza, yaliyomo katika Waraka wa Kipapa, uliotolewa baada ya Sinodi ya Pili ya Maaskofu Maalum kwa ajili ya Kanisa barani Afrika , "Waraka wa Dhamana ya Afrika (Africae Munus)", kwa kuzingatia kwamba changamoto ya amani, haki na maridhiano, leo hii ni hitaji la kidharura zaidi kwa wana wa Afrika.


Utamadunishaji Injili katika muono wa amani , haki na maridhiano , na nini leo hii, Neno la Mungu kupitia Yesu Kristu linasema, katika mitazamo ya dunia iliyomezwa na utamaduni wa chuki, vurugu, na ukandamizaji, umaskini na miuundo mbovu ya kijamii, na ikiwepo chemko la imani na tumaini, inabaki kuwa changamoto kwa Kanisa Afrika.


Tatizo linabaki kuwa lilelile kutamadunisha Injili na Ukristu, katika mtazamo wa ukombozi , amani, haki, upatanisho kama ilivyo elezwa katika Mtaguzo Mkuu wa Pili wa Vatican na Sinodi ya Maaskofu maalum kwa ajili ya Afrika ya mwaka 1994, katika roho ya uinjilishaji mpya. Kwa kifupi, maneno yenyewe “Uinjilishaji mpya " bado ni dhana inayohitaji ufafanuzi zaidi. Maaskofu wa Afrika, tuliozungumza nao, kwao walitaja wazi kwamba, ni wazi Mkutano huu ulioitishwa na Khalifa wa Mtume Petro, kama baraza la Sinodi juu ya Uinjilishaji Mpya, katika mwaka wa imani, ni sehemu kubwa ya mpango wa kidunia, unaolenga kufanikisha utamadunishaji Injili, ambayo leo hii, ni kati ya changamoto kubwa zinazokabili Kanisa kwa ujumla.


Hivyo basi, ni muhimu kuzingatia maswali yasiyokoma kuulizwa katika mabadiliko haya, nini maana ya kukutana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristu, na mafundisho mengine sadikifu ya Kanisa. Na ni vyema kukumbuka kwamba, katika taratibu za kutoa ufufunuzi juu ya dhana hizi , na maneno mengine, kwamba kila mara huwekwa katika hatari maelezo kupotoshwa, kutokana na lugha zinazotumiwa na wake kwa waume wa nyakati zote, hasa katika kueleza maana ya Ufunuo katika wingi wa tamaduni na utambulisho wake. Kwa maneno mengine, si tu matatizo ya kutafsiri mahusiano kati ya ishara za imani, lakini kinacho hitajika zaidi ni ufafanuzi wa kiteolojia katika dunia yenye kuwa na mwelekeo wa kutaka kufinyanga finyanga tafsiri aminifu za imani hasa katika kisingizio cha ubunifu mpya wa kueneza Injili.

Na katika fikira mpya za Utume wa wafuasi wa Kristu wa nyakati hizi, ni njia inayofaa kutimiza utume wa Kanisa kikamilifu, katika dunia inayozidi kusonga mbele katika malimwengu na utata wa kutoa maana zake halisi, kitamaduni, kiuchumi, kisiasa, kieneo , kidini na kiroho. Basi kwa mtazamo huo, kile ambacho siku za nyuma kilionekana kuwa ni kwa ajili ya Kanisa la Afrika na Asia, kwa wakati huu imekuwa ni utume wa Kanisa zima kutamadunisha, katika lengo la kuionyesha upya sura na utambulisho wa Mkristu katika dunia ya kisasa.


Kwa mara ya kwanza, neno utamadunisho lilitajwa mwaka 1977, katika "Ujumbe kwa Kanisa zima la Ulimwengu, wakati ilipofanyika Sinodi ya Maaskofu ,juu ya Katekesi", na kisha kuwekwa rasmi katika waraka wa kumi na saba, (kulingana na tathmini iliyofanywa na msomi wa Hervé Carriier kwa neno hilo). Baada ya Baraza kutoa tafasiri ya utamaduni, majadiliano na Uinjilishaji, kulitolewa nyaraka mbili za kitume za Kipapa , ule wa Papa Paulo VI na Yohane Paulo II, pia hotuba nne , zikifuatiwa na nyaraka za kitume tatu za Papa Yohane Paulo II juu ya suala hili, Waraka wa Ukombozi“ Redemptoris” na ule wa Kanisa Barani Afrika”ecclesia in Africa”. Kwa kuzingatia kwamba , utu wa mtu huonekana katika utamaduni wake , kama ilivyolezwa katika mtaguzo Mkuu wa Pili wa Vatican, Papa Yohana Paulo II alisema, utamadunisho ni "moyo, njia na mwisho wa uinjilishaji mpya ".

Ni wazi, hili linahitaji imani. Na utume huo si kwa ajili ya kanisa Barani Afrika na Asia peke yake. Lakini pia ni changamoto kwa Askofu wa Roma, katika umuhimu wake wa kuonyesha mfano katika juhudi za kutamadunisha Ukristu, kihistoria na kitamaduni katika nyakati zetu na miaka hamisini baada ya kutolewa kwa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Kwa kifupi utamadunishaji si tu juu ya wengine wanaoishi Kusini mwa tufe la dunia. Bali sasa nii hitaji la kanisa zima la ulimwengu, kuitamadunisha imani ya Kanisa la Kristu kwa watu wote duniani. Ni ufanikishaji wa mabadiliko thabiti ya imani ndani ya kanisa.


Kwa maana hiyo , mpango wa utamadunishaji unakuwa ni moja ya vipengere muhimu katika utendaji wa Injili ya Yesu Kristu Mkombozi, dhidi ya mambo ya kidunia leo hii, hasa katika Mikoa ya EuroKaskazini Magharibi mwa Ulaya . Hapa ambapo baada ya miaka elfu mbili ya historia ya Ukristu na miaka hamsini ya Mtaguzo Mkuu wa Pili wa Vatican , kunaendelea kuwa na mbadiliko yanayo shusha hadhi ya imani katika utendaji, iwe kwa mtu binafsi, au jumuiya, imani ikifanywa kama vile ni hoja ya kisiasa, kutokana na ukweli kwamba, utamaduni wake umekuwa ni wa kimagharbi zaidi, kuliko utamaduni wa kikristu. Na zaidi sana ,kutokana na ukosefu wa uvumilivu, kwa mataifa haya makongwe katika malezi ya Kikristu na mapokeo ya utamaduni wa tangu kale kama kielelezo cha utamaduni wa watu wa Ulaya.


Na sasa, si kama bahati mbaya, Baba Mtakatifu, kuitishwa kwa Baraza la Sinodi, akiwa pia mmoja wa wale walioshiriki katika Baraza la mtaguzo Mkuu wa Pili wa Vatican, na msharika wa karibu wa Yohane Paulo II. Benedikto XV1 anasema, changamoto hii ya Uinjilishaji mpya, inadai kazi zake zufanyike kwa maongozi ya kina ya kiroho, ambayo yanayoonekana kwa miongo mingi, katika mitazamo ya kikanisa, kutaka kutoweshwa badala ya kuwa dhana ya uwajibikaji na ushirikiano katika Kanisa. Uwajibikaji na ushirikiano ili kwamba, Kanisa liweze kuonyesha katika dunia ya leo, ishara za kanisa kama ni nyumbani na mahali pa maridhiano na umoja katika majadiliano na kufurahia uhuru kama wana wa Mungu na pia kuwa kioo cha ubinadamu kama alivyoeleza Papa Yohane Paulo 11, kama familia ya Mataifa.

Tayari karibu na mwisho wa Utawala wa Papa Yohane Paulo II, kulikuwa na nia hizi za kuonja furaha ya usharika wa kikanisa. Na katika mapambazuko ya Millenia, Papa Yohane Paulo 11 alitoa wito kwa Wakristu kuipokea changanomoto hii ya imani tangu mwanzo wa millenia ya tatu : kulifanya kanisa kuwa nyumbani na shule ya umoja.


Katika uwanja wa utamadunisho, basi makanisa ya Afrika na Asia yanakuwa na mengi ya kuchangia katika hoja hiyo. Na hivyo inakuwa suala la kuukubali ukweli kwamba, Makanisa makongwe katika Ukristu , ambayo kwa karne nyingi, yamedhani kwamba, dhana ya utamadunisho na ujenzi wa utambulisho wa Mkristo , ni kwa ajili ya makanisa machanga, yanayoitwa makanisa ya Misioni,yaliyotakiwa kusikiliza na kufungua roho yake katika uwajibikaji na ushirikiano wa kikanisa, katika hadhi yakwua sawa kama watoto wa Mungu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mmoja. Sasa Kanisa kwa ujumla, lina hitaji la kutazama utabiti wa imani yake katika mitazamo ya kutamadunisha Injili upya, ktika hitaji hilohilo la kujenga umoja na ushirikiano katika imani.


Suala ni jinsi msukumo huu mpya katika utamadunishaji Injili unavyoweza kuivuka mipaka ya malimwengu,na kuwa ni utamaduni wa maisha ya waamini wa Kanisa lote la ulimwengu kwa nyakati hizi zetu. Kwa mtazamo huo, hakuna tena sababu za kuuliza maana halisi ya tafasiri ya Neno la Mungu katika utamaduni mahalia. Jibu na tafasiri yake, vinakuwa ni muhimu , katika kusindikiza mijadala, umoja na uwajibikaji, katika kuifikia hatima ya ubinadamu huu ambao tayari kwa maneno ya Papa Paulo V1, ni safari ya hija ya Kanisa hapa duniani. Je kwa uelewa huo, bado tena kuna sababu za kuuliza manufaa au tafsiri yake ya Neno la Mungu katika hali za kitamaduni?


Ni matumaini ya Sinodi kwamba, itaweza kuamsha dhamiri katika utambuzi wote kwamba, kama binadamu, Mungu amemjalia kila mmoja wetu masikio mawili , macho mawili na kinywa. Hoja ni: kati ya hivi tutatumia nini zaidi?


Wale wenye haraka ya kutoa jibu, watajibu kama yanenavyo maneno ya hekima, mwenye haraka huishia kutafuna ulimi wake. Njia pekee ya kuondokana na kurudia rudia utendaji wa miaka elfu mbili ya historia ya Ukristu ,ni kujifunza upya kusikiliza kwa moyo thabiti na ushirikiano, kwa ajili ya uwajibikaji katika kuiishi Injili, ili Injili isipoteze onjo lake.

Kwa mtazamo huo , Kanisa , kama alivyo eleza André Manaranche na Jean-Marc Ela, linaalikwa kutafakari kwa uangalifu linachosema na kueleza kwa upole, likiwa limejawa na imani ya kina kwa Yesu Kristu Mkombozi.


Mhariri Lopes Filomeno, Idhaa ya Kireno kwa Afrika, Radio Vatican.










All the contents on this site are copyrighted ©.