2012-11-02 09:02:05

Papa kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia kutoka sehemu mbali mbali za dunia: 2011 - 2012.


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumamosi tarehe 3 Novemba 2012, anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwaka 2011 hadi Oktoba 2012.

Takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha Mwaka uliopita, kuna jumla ya Makardinali 10 waliofariki dunia. Kuna Jumla ya Maaskofu 143, ambao pia wametangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko wa wafu na maisha ya uzima wa milele. Kati ya Maaskofu hao, kuna jumla ya Maaskofu 21 kutoka Afrika.

Maaskofu wafuatao ni wale waliofariki dunia kutoka katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA:

1. Askofu Augustini Misago wa Jimbo Katoliki Gikongoro, Rwanda: 12 Machi 2012.
2. Askofu mstaafu Joseph Nduhirubusa wa Jimbo la Ruyigi, Burundi: 16 Julai 2012.
3. Askofu Pascal W. Kikoti wa Jimbo Katoliki Mpanda, Tanzania: 28 Agosti 2012.
4. Askofu mstaafu Patrick A. Kalilombe, Jimbo Katoliki Lilongwe, Malawi: 25/9/ 2012
5. Askofu mstaafu Joseph B. Williger, Jimbo Katoliki Jinja, Uganda, 30/9/ 2012.
6. Askofu mstaafu Felix E. Mkhori, Jimbo Katoliki Lilongwe, Malawi, 17/10/ 2012.







All the contents on this site are copyrighted ©.