Vatican na Croatia zafanya kumbu kumbu ya miaka 20 ya uhusiano wa Kidiplomasia kwa
Kongamano na Hija ya Kiroho mjini Roma
Baraza la Maaskofu Katoliki Croatia, katika mkutano wake uliohitimishwa hivi karibuni,
pamoja na mambo mengine limejadili kuhusu kumbu kumbu ya maadhimisho ya miaka ishirini
tangu Croatia na Vatican zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia. Mkutano huu umehudhuriwa
pia na Askofu mkuu Alessandro D'Errico, Balozi wa Vatican nchini Croatia.
Maaskofu
wamezungumzia kuhusu hija ya kikazi itakayofanywa na Waziri mkuu wa Croatia Bwana
Zoran Milanovic pamoja na kushiriki katika Kongamano litakalojadili kuhusu uhusiano
wa kidiplomasia kati ya Vatican na Croatia katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita;
kongamano ambalo linafanyika hapa mjini Vatican tarehe 29 Oktoba, 2012.
Baraza
la Maaskofu Katoliki Croatia litafanya hija ya kichungaji mjini Roma, ili kumshukuru
Mungu kwa matunda ya uhusiano uliopatikana kati ya nchi hizi mbili pamoja na kuadhimisha
Mwaka wa Imani, uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na
sita, hivi karibuni.