2012-10-29 09:18:09

Kanisa Katoliki Malawi linaomboleza Kifo cha Askofu mstaafu Felix Eugenio Mkhori


Askofu mstaafu Felix Eugenio Mkhori wa Jimbo Katoliki la Lilongwe, Malawi amefariki dunia hapo tarehe 27 Oktoba, 2012, baada ya kuugua kwa muda mfupi na anatarajiwa kuzikwa kwenye Kanisa kuu la Chikwawa, Jumatano tarehe 31 Oktoba, 2012 majira ya saa 3:30 asubuhi.

Marehemu Askofu Felix Eugenio Mkhori alizaliwa kunako tarehe 24 Agosti 1931, katika Jimbo kuu la Blantyre, Malawi. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, alipewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 8 Septemba 1961. Aliteuliwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chikwawa hapo tarehe 29 Septemba 1977 na kuwekwa wakfu tarehe 8 Januari 1978.

Tarehe 23 Januari 2001 alihamishiwa Jimbo Katoliki la Lilongwe. Baada ya kuitumikia Familia ya Mungu kwa busara na majitoleo makuu, aling'atuka madarakani kunako tarehe 4 Julai 2007.







All the contents on this site are copyrighted ©.