2012-10-24 16:07:27

Sinodi yaanza kazi ya kuunganisha mawazo na maoni ya Mababa wa Sinodi.


Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu , Jumanne , kikao chake cha kumi na tisa, juu ya Uinjilishaji Mpya, kiliendelea na kazi za kuungaisha mawazo yaliyotolewa na wajumbe mbalimbali wa sinodi hiyo , ili kutoa rasimu ya mwisho, ambayo hatimaye itafanyiwa marekebisho na kupigiwa kura hapo Jumamosi ya wiki hii, kabla ya kuhitimisha vikao vya sinodi.

Pia katika kikao hicho cha Kumi na Tisa, Mababa wa Sinodi walitoa ombi la kuachiwa huru wamisionari tatu, waliotekwa nyara , Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Na pia walisisitiza kwamba , wataendelea kushikamana na watu wenye mapenzi mema Syria, kufanikisha amani na utulivu kwa raia wa Syria. Nababa wa Sinodi wanasema, kwa hali yoyote ile , hakuna kitakachoweza kusitisha azma yao, katika kushikamana na watu wa Syria na wale wanaotafuta ufumbuzi wa migogoro wa Syria kwa njia ya amani. ..

Mababa wa Sinodi, licha ya maandalizi ya rasimu ya sinodi, bado pia wanaendela kukusanya michago na mapendekezo .

Isabela anasema, mtazamo wa jumla wa Sinodi, unaonyesha kwamba, uinjilishaji ni utume wa Kanisa, hasa katika dunia ya iliyo limwengushwa na utandawazi, inakuwa ni changamoto muhimu kupambana na madhulumu ya kidini au watu kutojali ya dini yenyewe. Kwa mazingira haya , utetezi wa uhuru wa kidini na haki msingi za binadamu, inakuwa ni sehemu ya Uinjlishaji kwa sababu Injili yenyewe ni utangazaji wa ujumbe wa amani , unaosaidia mtu kuepuka upweke unaoletwa na dunia ya kisasa.

Miongoni mwa mambo mengine yaliyojadiliwa kwa kina na sinodi ni umuhimu wa matumizi sahihi ya vyombo vya habari na wataalamu wa malezi na majiundo katika maadili ya Kikristo. Pia njia za uinjilishaji kupitia uzuri na sanaa takatifu.
Maaskofu pia, wamehimiza utetezi wa watu wahamiaji na fursa ya kutangaza injili wanayoweza kupewa. Na utakatifu kama sehemu kubwa ya uinjilishaji mpya, na umuhimu wa kufanya rejea katika mafundisho ya kijamii ya Kanisa na Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican, kama dira ya juhudi zote za uinjilishaji mpya.

Pia kulikuwa na marejeo ya Katekesi, kama kipengere muhimu katika kuendeleza elimu ya imani kwa watu wazima. Huduma kwa maskini na wagonjwa katika mtazamo wa kuinjilisha kwa upendo, na sakramenti ya kitubio kama msingi wa hatua ya kichungaji ya Kanisa. Pia wajibu na ushirikiano wa walei –wakiwemo vijana , na utambuzi wa jukumu la wanawake, katika udumishaji wa imani hai na matumaini.

Isabella anaendelea kutoa muhtasari kwamba, Mababa wa Sinodi, pia wametazama kwa makina masuala ya familia na kutoa wito wa kusaidia familia, kama wakala wa kwanza wa uinjilishaji, na waliliangalia suala la talaka na kuoa tena. Na Makuhani na viongozi wa kanisa, kwamba, wanaitwa kuinjilisha kwa roho ya kina na kuyafahamu mambo ya kisasa, ili waweze kukabiliana nayo vyema katika maisha ya kila siku ya jamii. Na kwamba, parokia ni zawadi, zawadi kwa ajili ya Kanisa, na hivyo Mapadre wanapaswa kushirikiana vyema wanaparokia na kufanya kazi yao kwa jicho la kina la kitume.
Sinodi pia imeangalisha katika majadiliano kw amitazamo mnne, uekumeni, dini zingine, sayansi na imani, na wasio waumini. Msingi mkuu wa kwa wote katika majadiliano hayo , ni kuheshimiana, ushirikiano kwa ajili ya kukuza haki za binadamu, na zaidi hasa katika mahusiano na Waislamu.

Hatimaye, Sinodi ya Maaskofu, imetoa wito wa kudumishwa kwa asili ya mazingira na viumbe, ushuhuda wa imani na mshikamano wa kizazi hadi kizazi , na kwa Maria, Nyota ya Uinjilishaji, kwa njia ambayo kanisa inaweza kuwa nyumbani kwa wengi.

Wakati wa kufunga kikao hiki, Katibu Mkuu wa Sinodi, Askofu Mkuu, Nikola Eterovic, alisoma ya ombi la Askofu Luka Ly, Askofu wa Fengxiang, China, ambaye hivi karibuni, alituma salamu kwa Mababa wa Sinodi. Sinodi imejibu barua hiyo, ikitaja pia upendo mkuu kutoka kwa Baba Mtakatifu, akionyesha tumaini lake kwamba, katika Mwaka wa imani, uinjilishaji mpya utaweza kufanikishwa pia katika taifa la China.








All the contents on this site are copyrighted ©.