2012-10-24 15:54:46

Papa ateua Makardinali wapya sita.


Jumatano hii, Baba Mtakatifu Baada ya Katekesi yake kwa mahujaji na wageni, pia alitangaza majina ya sita ya Makadinali wapya wateule, watakaotajwa rasmi wakati wa Baraza la Makadinali hapo Novemba 24, 2012.
Makardinali wapya wateule ni
Mons.JAMES MICHAEL HARVEY, Padre Mkuu wa Kanisa la Kipapa la Mtakatifu Paulo nje ya kuta Roma.
Mwenye Heri BÉCHARA BOUTROS RAÏ, Patriarca wa Antiochia ya Maroniti (Lebanon);
Mwenye Heri BASELIOS CLEEMIS THOTTUNKAL, Askofu Mkuu wa Trivandrum ya Siro-Malankaresi (India);
Askofu Mkuu JOHN OLORUNFEMI ONAIYEKAN,wa Jimbo Kuu la Abuja (Nigeria);
Askofu Mkuu RUBÉN SALAZAR GÓMEZ, wa Jimbo K uu la Bogotà (Colombia);
Na Askofu Mkuu LUIS ANTONIO TAGLE, wa Jimbo kuu la Manila (Filippine).
Papa alitangaza na kuwaomba waamini watolee sala zao kwa ajili ya Makardinali wapya, kuomba msaada kwa Mama Bikira Maria , ili waweze kulipenda kanisa kwa ushupavu na majitoleo kwa ajili ya Yesu Kristu na Kanisa lake.







All the contents on this site are copyrighted ©.