2012-10-23 15:22:59

Miaka 22 ya Waraka wa "Redemptoris Missio"


Jumatatu , Mama Kanisa alifanya kumbukumbu ya kiliturujia kwa Mwenye Heri Yohane Paulo II, ambaye mafundisho yanaendelea kumulikia mengi, ikiwemo kazi za uinjlishaji mpya.

PapaYohane Paulo 11, ndiye kwa mara ya kwanza, alitoa wazo la kuwa na uinjilishaji mpya , wakati wa ziara yake ya kwanza ya Kichungaji nchini mwake Poland, mwaka 1979. Mafundisho yanayo endelea kuwa msaasda mkubwa kwa Maaskofu wa Kanisa la Ulimwengu, hata katika Mkutano wa Sinodi inayoendelea sasa , juu ya Uinjilishaji mpya.

Mwenye Heri Yohane Paulo 11 ,alizitazama changamoto za Kanisa leo hii, hasa katika mataifa kongwe katika Ukristu, ambamo Ukristu umezoeleka kama ni sehemu ya utamaduni wake wa siku nyingi, lakini hali halisi ya maisha ya watu, yanaonekana kujitenga nje ya misingi ya Ukristu.

Mwenye Heri Yohane Paulo 11, katika miaka hiyo ya 1979, akikabiliana pia na ukomunisti katika nchi yake , alisisitiza uinjilishaji mpya , katika millenia mpya kwamba, ni muhimu kuzingatia mafundisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican." Na kwamba, waamini wote wanapaswa kushiriki katika kazi hii, Maaskofu na makuhani, na watawa, na hasa walei.
Katika majadiliano yake ya Mei 18, 1981 na Maaskofu wa Italia, alisema , Uinjlishaji mpya , usielekezwe tu kwa watu binafsi, lakini iwe ni sehemu ya maisha ya utendaji mzima wa waamini mahalia, kulingana na hali zao mbalimbali, kimazingira, na kitamaduni na kijamii kwa ujumla, hasa katika malengo ya malezi na majiundo yanayoweza kuimairisha ukomavu wa imani, katika kutambua asili yote ya imani . Na hasa katika kuzingatia kwamba, ni hitaji la lazima kwa mfuasi wa Kristo, kuziiishi sakramenti na kujenga ushirika na Yeye Kristu, ambaye ndiye asili maisha ya upendo na huduma.

Kwa ajili hiyo , mwaka 1990, alichapishaji waraka,” Utume unaokomboa (Redemptoris Missio)”. Katika waraka huo, Mwenye Heri Yohane Paulo 11, anasema, “Makanisa kongwe , yanakabiliana na kazi ya uinjilishaji mpya," na si tu kupeleka Injili katika mataifa yasiyomjua Kristu bado, lakini hata ndani mwake yenyewe, kutokana na ukweli kwamba, katika mataifa hayo , sasa wengi wanaonekana kusahau maadili ya Ukristu.

Miaka 22 iliyopita, waraka wa Papa Yohane Paulo 11 juu ya Uinjilishaji Mpya kwa Utume wa Mataifa, kama ilivyokuwa tangu mwanzo wa Utawala wake wa Kipapa, bado unaonyesha haja ya juhudi mpya za kuinjilishaji, kama hatua ya kukabiliana na changamoto, katika Millenia ya Tatu.








All the contents on this site are copyrighted ©.