Katekesi ni muhimu katika majiundo na ukomavu wa imani kwa wafuasi wa Kristu
Hili ni wiki la Mwisho la Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Uinjilishaji mapya. Jumatatu
kazi za Sinodi kwa ajili ya Uinjilishaji mpya , zilifanyika katika hali ya faragha,
kwa ajili ya uunganishaji mawazo na mapendekezo yaliyo kwisha tolewa. Sinodi inafungwa
jumapili ya wiki hii, 28 Oktoba kwa Ibada ya Misa.
Taarifa zinasema, michango
mbalimbali ya maoni na ushauri iliyotolewa na Mama katika siku hizi za Sinodi, imeonyesha
umuhimu wa juhudi mpya katika Uinjilishaji kuangalishwa kwa watu wazima pia , ambao
wengi wameonekana au mwelekeo wa kusahau jukumu lao, kama waamini kuirithisha misingi
ya imani, elimu na shuhuda, kwa kizazi kipya cha vijana.
Na kwa namna pekee
, Mons. Satanislaw Gadecki wa Poland, alitoa uzoefu wa shule ya Katekesi ya watu wazima
,kama sehemu ya uinjilishaji mpya, nchini mwake. Na kwamba mpaka sasa bado wanashakia
kuchukua hatua ya kutoa katekesi kwa watoto na vijana, kabla ya kuwakiria kwanza
watu wazima, kwa dhana kwamba, katekesi kwa watoto, itakwua ni matunda na maendeleo
ya Katekesi kwa watu wazima.
Na ameasa kwamba, mafanikio katika makundi yote
mawili, watu wazima na vijana, yanategemea sana watu wazima wenyewe , tabia na maisha
yao. Kwa mara nyingi, imani haba kwa mtu mzima huharibu pia mbengu nzuri ya Imani
iliyo pandikizwa kwa vijana. Uenezaji wa Imani na utendaji wake , usitokana na iamni
yamtu mzima , kwa vijana hutoweka mara.
Aidha Mons. Stanslaw Gadecki ameonyesha
kujali jinsi watu wazima wanavyokosa muda wa kukakaa na watoto wao, kutokana na hali
halisi za ukali wa maisha, kwamba, watu wazima wanalazimika kuishi maisha ya uchugu
wa kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi, ili kukidhi mahitaji ya familia. Wengi badala
ya saa nane, wanafanya zaidi ya saa 12 au hata 14 kwa siku, na hivyo hurejea nyumbani
jioni wamechoka na hawana muda wa kukaa na watoto wao, kuwaelimisha yale wanaoyajua
ikiwemo imani yao.
Pamoja na changamoto hii, kwa ajili ya kuimarisha uelewa
wa imani kwa watu wazima ili waweze kuirithisha kwa watoto wao, inakuwa ni jambo muhimu
kutoa Katekesi kwa watu wazima. Na hiyo ndilo lengo la shule ya makatekista walei,
na watu wazima , kupata uzoefuzaidi katika imani yao na kujenga ukomavu unaostahili.
Na kwamba wameanzisha shule ya Katekesi kwa watu wazima , baada ya kugundua kwamba
haiwezekani kuwa na Makatekista na shuhuda thabiti bila ya maandalizi. Na uzoefu umeonyesha
kwamba, lugha ya walei katika kuieneza imani kwa watu wazima walei ina shawishi zaidi,
kuliko lugha ya Mapadre.