2012-10-22 15:44:50

Wakoptic wako tayari kuchagua kiongozi mpya


Wakoptic wa Alexandria wako tayari kuchagua Kiongozi wao mpya hapo tarehe 29 Octoba 2012. Uchaguzi huo, umepangwa kufanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Paulo la Abbasiya .
Msemaji wa Kamati inayosimamia upigaji wa kura alitangaza hilo siku ya Jumapili . Na kwamba, majina matatu yatakayopata kura nyingi katika duro ya kwanza ya uchaguzi, yatatangazwa mara , ili yapigiwe tena kura hapo tarehe 4 Novemba na matokeo yake pia kutangazwa siku hiyohiyo.
Wanahabari wamearifiwa kwamba, hawataruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa kupigia kura, ila wataweza kufuatilia tukio hilo kupitia video zitakazokuwa zimewekwa katika Kanisa kuu hilo. Na propaganda hazitaruhusiwa isipokuwa maelezo ya wagombea.
Kanisa la Kikopitic la Alexandria linachagua kiongozi mpya, kufuatia kifo cha kiongozi wake , Patriaki Papa Shenouda III, aliyefariki mwezi March, akiwa na umri wa miaka 88.
Marehemu Papa Shenouda III, aliongoza Upatriaki wa Kanisa la Kiotodosi la Alexandia kwa muda wa miaka 40 , katika kipindi kigumu cha maonevu na mivutano kutoka kundi kubwa la Waislamu, anaowazunguka.










All the contents on this site are copyrighted ©.