Chagua kiongozi bila ya kujali dini, kabila au mahusiano - Kasisi ahimiza.
Jambo la kwanza kabisa katika kumfikiria kiongozi bora ni uadilifu wake katika kuainisha
dini na siasa. Na hamu za kumchagua kiongozi asiyekuwa mwaminifu eti kwa sababu
tu ni wa dini yako, hiyo ni dhambi kwa dini ya kweli. Ni wito uliotolewa na Padre
Wilybard Lagho, Kasisi wa Mombasa na Rais wa Baraza la Pwani linalo waunganisha wakuu
wa dini (CCC), katika kutafakari juu ya uchaguzi ujao wa urais utakao fanyika nchini
Kenya mwaka ujao.
Padre Lagho ameitaja nafasi ya uchaguzi, kuwa fursa kwa
wapiga kura , kuchagua viongozi waaminifu, bila kujali hadhi yai kifedha, kabila au
dini au mahusiano. Ameuita uchaguzi wa viongozi wa kisiasa, kuwa mtihani wa uadilifu
kwa wapiga kura wenyewe. Maelezo ya Padre Lagho yamenukuliwa na shirika la Fides,
ambamo amerejea kumbukumbu ya mapigano ya hivi karibuni, yaliyogusa madhehebu ya
kidini mjini Mombasa. Fr. Lagho, amesema , Koran na Biblia, vyote huwataka Wakristo
na Waislamu kuishi kwa amani na ujirani mwema.
Na kwamba, ni jambo lisilo wezekana
sasa , kwa ukanda wa pwani, hasa katika jiji la Mombasa, ambako Waislamu na Wakristo,
wameishi karne hadi karne kwa hali ya utulivu na amani licha ya tofauti za kidini,
sasa kuibua utengano, kati ya jumuiya hizi mbili. Ameeleza na kurejea maelezo ya
Mtume Mohammed juu ya jirani mwema kwamba, Jibrael (Gabriel) alipendekeza kuwahudumai
majirani kwa wema na upole(Sahih Bukhari zote - kitabu cha Ahkaam). "
Na kwa
mfano wa Msamaria mwema uliotolewa katika Kitabu cha Injili, Wakristu wanafundishwa
kuwahudumia majirani na maskini bila kujali itikadi zao za kijamii, kikabila na
kidini (Luka 20, 25-37)."
Padre Lagho alimalizia ujumbe wake kwa kuwataka
viongozi wa dini, kuungana na kuhamasisha wapiga kura kuchagua viongozi waaminifu
ambao watafanikisha watu wengi zaidi kufurahia uhuru wao dhidi ya minyororo ya rushwa
na mafisadi