Wakristo simameni kidete kulinda mali zenu pamoja na kutetea haki zenu msingi dhidi
ya nyanyaso na madhulumu ya kidini!
Askofu Mkuu Josephat L. Lebulu wa Jimbo Kuu Arusha, Tanzania amewataka watanzania
kwa namna ya pekee kujitokeza kuchangia maoni yao katika mchakato wa Katiba Mpya ya
Tanzania, kama sehemu ya utekelezaji wa dhamana yao kama raia wa Tanzania.
Askofu
Mkuu Lebulu amesikitishwa sana na vitendo vya dhuluma na uvunjifu wa misingi ya uhuru
wa kuabudu, haki na amani vinavyoendelea kujitokeza nchini Tanzania, licha ya Kanisa
kuongeza jitihada za kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini na kukazia umuhimu
wa kufuata na kuzingatia utawala wa sheria, lakini haki, amani na utulivu sanjari
na mustakabali wa taifa, vimeendelea kuwekwa rehani na baadhi ya Waamini wachache
wanaoendeleza sera za ubabe na nguvu dhidi ya Wakristo nchini Tanzania.
Askofu
Lebulu anawataka sasa Wakristo nao kusimama kidete kupinga dhuluma na nyanyaso na
ukosefu wa misingi ya haki wanayotendewa nchini Tanzania kwa kuhakikisha kwamba, haki
yao ya kuabudu inaheshimiwa na kuthaminiwa na Waamini wa dini nyingine nchini humo.
Kanisa haliwezi kukaa kimya na kuona watu wanadhulumiwa na mali yake inateketea kwa
visingizio vya udini. Zaidi anafafanua kama ifuatavyo: