2012-10-15 10:39:11

Msijaribu kuubinafsisha mchakato wa Mtumishi wa Mungu Julius K. Nyerere kutangazwa kuwa Mwenyeheri! Ni Hatari!


Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar ambaye pia ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kutoka Barani Afrika kuhakikisha kwamba, wanatafuta zaidi mafao ya wengi kwa njia ya kujitoa bila ya kujibakiza na kamwe wasigubikwe na tamaa ya kutafuta utajiri, sifa na masilahi yao binafsi kiasi cha kusahau wajibu na dhamana waliyokabidhiwa na Kanisa pamoja na Jamii kwa ujumla wake.

Kardinali Pengo amewaonya baadhi ya watu wanaotaka kubinafsisha mchakato wa kumtangaza Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya sifa na utukufu wao binafsi kuwa mwelekeo wa namna hii unaojionesha hata ndani ya Kanisa na miongoni mwa wanasiasa ni hatari katika zoezi zima la mchakato wa Mwalimu Nyerere kutangazwa kuwa Mwenyeheri, hatua ambayo kwa sasa iko katika ngazi ya Kijimbo. Mwalimu Nyerere awe ni mfano bora wa kuigwa kwa majitoleo yake kwa ajili ya mafao ya wengi, ukuu na utakatifu wake, viwe ni sifa kwa Mwenyezi Mungu aliyetenda makuu katika maisha ya Mwalimu.

Kardinali Pengo ameyasema hayo wakati akitoa salam kwa watanzania na watu wenye mapenzi mema, waliohudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu, kama sehemu ya kumbu kumbu ya miaka kumi na mitatu, tangu Mtumishi wa Mungu Mwalimu Julius K. Nyerere alipofariki dunia, Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu Mkuu Protas Rugambwa, Katibu mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimissionari.

Zifuatazo ni salam na matashi mema kwa watanzania kutoka kwa Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. RealAudioMP3







All the contents on this site are copyrighted ©.