2012-10-13 10:54:06

Furaha katika hali ya unyenyekevu


Padre Federico Lombardi, Mkurugenzi wa vyombo vya mawasiliano Vatican na Msemaji wa Papa, katika tahariri yake ya wiki hii, ametazamisha kwa makini maelezo ya Papa Benedikto XV1, aliyoyatoa tarehe 11 Oktoba 2012, kwamba miaka 50 iliyopita ,katika tarehe hiyo, akiwa Padre, pia alikuwa miongoni mwa watu waliofurika katika uwanja huu wa Mtakatifu Petro, wakiwa wamekaza nyuso zao juu kulitazama dirisha maarufu duniani, wakisumbiri kumwona na kusikiliza hotuba ya Mtagulizi wake , Papa Yohane XXIII.

Padre Lombardi ameendelea kueleza kwamba, katika tarehe hiyo 11 Oktoba 1962, Padre Joseph Ratzinger , akiwa amejawa na moyo safi wa kipadre, hekima na upendo , pia alilitazama dirisha hilo kwa hamu kubwa ya kumwona Papa Yohane XIII. Na leo hii, Padre huyo, ndilo anaye subiriwa kwa hamu atokee katika dirisha hilio hilo, alilolitazama yeye kwa hamu, kusikiliza ujumbe unaotolewa na Papa kwa makusanyiko ya watu, wanaomtazama tokea chini. Ujumbe wa imani, uliowasilishwa kwa fumbo la Mungu, Mungu hai asiye na nyakati wala kipimo, Mungu wa milele yote. Mungu, aliyekuwa kipaumbele cha kwanza katika majadiliano yote ya Baraza la Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, lililomalizika na wito kwa binadamu, kurekebisha maisha na kuzamisha ukweli katika utendaji.

Mungu ni historia yetu , na historia ya Kanisa. Ndiye aliye furaha na matumaini , huzuni na mateso yote ya binadamu , hata yale ya wafuasi wa Kristu, ndivyo unavyoanza ukurasa wa waraka wa mwisho wa hati ya Baraza. Ni maeelezo yanayotakiwa kusomwa kwa mwanga wa fumbo la Kiinjili, mfano maana ya samaki wabaya na nyavu. Maelezo juu dhambi ya kijicho na ubaya ,vilivyogubikwa katika mifumo ya dhambi, yenye kuumiza ubinadamu na maisha ya kila mmoja wetu. Lakini pia maelezo ya neema ambayo hutenda kazi zake kimyakimya na kuijionyesha kama mwali mdogo wa moto wa wema, huruma na ukweli , kama ilivyoonekana miali ya mishumaa mishumaa mingi nyakati za usiku katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro wakati wa giza la usiku. Lakina furahi iliweza kusikika , furaha katika unyenyekevu, furaha ya kweli, yenye kutambulisha uwepo na utendaji wa Roho Mtakatifu wa Bwana ambaye yupo pamoja nasi, na tena kwa nguvu na uaminifu wote. Furaha tulivu mfano wa mwali mdogo wa wema na ukweli, ambao nguvu ya utendaji wake hupasua kuta zote za giza nene na kuonekana.

Padre Federico Lombardi amemelizia tahariri akisema, Papa Benedikto XV1, ameonyesha mwelekeo wote , wa jinsi ya kuuishi mwaka wa Imani.Tarehe 11 Oktoba, alitokea dirishani na kuitazama bahari ya watu waliofurika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kuwahutubia na kumalizia na maneno ya Mtagulizi wake Yohane XXIII, ”Nendeni nyumbani , mkawakumbatie watoto wenu na mseme kwao , ni buso kutoka kwa Papa . Busu jepesi lililojaa upendo wa Mungu . Na ndivyo mwaka wa Imani unavyoanza”.








All the contents on this site are copyrighted ©.