2012-10-12 16:05:54

Mchakato wa imani si kupungukiwa na imani- Papa


Baada ya sherehe za kuzinduliwa kwa mwaka wa Imani, Maadhimisho ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na miaka 20 ya Katekisimu Katoliki, Ijumaa hii , vikao vya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Uijilishaji mpya, vimendelea kama ilivyopangwa hapa Vatican.

Baba Mtakatifu Benedikto XV1, asubuhi alihutubia Sinodi, na kutoa shukrani za dhati kwa umoja na mshikamano mzuri, ulioonekana wakati wa kuzindua maadhimisho hayo. Amesema ni Ibada ya Ekaristi pekee yenye kuwa na uwezo wa kuunda umoja huo thabiti. Na kwamba, ulionyesha umoja usiotanguka katika dekania ya maaskofu, walio jumuika pamoja na Khalifa wa Mtume Petro.

Baada ya shukurani za jumla, kwa namna ya Pekee alirejea hotuba ya Kardinali Arinze ,ya wakati wa sala, ambamo aliwataja kwa upendo, Maaskofu karibia sabini ambao bado hai, walioshiriki katika kazi ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Papa amesema, wengi wao bado wanazo kumbukumbu nyingi za Mkutano huo, na wana mengi yanayowagusa ambayo muda wote yamekuwa wakiwasukuma mbele kudumisha mshikamano na Khalifa wa Mtume Petro hadi sasa, wakiwa tayari hta kutolea sadaka maisha na mateso yao.

Papa amesema, kuna wengi na mengi ya kukumbuka katika kipindi hicho, lakini kati ya yote, alirejea maneno ya Mwenye Heri Yohane XXIII, wanayo yalirudia mara kwa mara katika kazi hizi za Sinodi, nao ni mchakato unaolenga kuboresha imani na uinjilishaji mpya.

Kwamba, furaha iliyoonekana Jumatano hii, mtu anaweza kupata wazo kwamba imekuwa ni furaha ya tangu kipindi cha miaka hamsini iliyopita, wakati kufunguliwa kwa Mtaguso Mkuu ulipozinduliwa hapo 1962, hili si kweli kwa kuwa wakati wote si wa furaha.
Papa amesema, pengine majadiliano juu ya hili yanaweza kuchukua muda wa saa nyingi kutoakana na kinzani katika maoni, lakini anaamini kwamba, maneno ya Mwenye Heri Yohane XXIII, bado ni sahihi, kwamba, . Ukristo haipaswi kuonekana kama "kitu cha zamani," au cha mpito, na wala jambo la kubadilika badilika katika muonekano wake au mbele ya macho ya watu, kwa sababu Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele (taz. Ebr 13:08). Ukristo ni alama na uwepo wa Mungu wa milele, Yeye aliye Mwanzo na mwisho wa nayakati zote.

Kwa ajili hii, Ukristo daima ni mpya. Papa alieleza na kulinganisha na mbegu ndogo ya haradali iliyotajwa katika Injili, ambayo hukua na kutoa matunda yake. Ukristo ni mti ni wa milele "unaobaki kijana muda wote.

Kwa maana hiyo, mijadala inayoelga "kuboresha "utendaji katika kuieneza Imani ya Kikristu, haimaanishi kuvunja mapokeo, bali ni kuonyesha maendeleo na uhai wake; haimaanishi kupunguza imani, au kupungua kwa utendaji wa nyakati katika kipimo cha binadamu , bali ni kinyume chake : kama walivyofanya Mababa Baraza, waliobaki hai leo hii, kuuonyesha Ukristu katika kipimo cha maisha ya Mkristu, kama sharti katika nyakati hizi zetu , kuionyesha “leo" ya Mungu”.

Papa ameendeela kusema, Baraza ni wakati wa neema ya mafundisho ya Roho Mtakatifu kwamba Kanisa, katika safari yake kwa njia ya historia, daima linapaswa kuzungumza na mtu wa kisasa. Lakini hii linawezekana tu kufanywa na wale wenye kuwa na nguvu zinazotokana na kujizamisha kwa kina katika mizizi ya kimungu , wakijiruhusu kuongozwa Nae na kuishi kwa usafi wa imani yao,. Na si kwa wale ambao hufuata upepo kwa muda na baadaye kuchagua njia ya starehe kulingana na matwaka yao.

Papa ameasa kwamba, Baraza la Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican , liliweka bayana Katiba na kanuni za Kanisa , kama ilivyoelezwa katika waraka wa Mwanga wa Mataifa “Lumen Gentium"), kipengere No. 49, kwamba wote katika Kanisa wameitwa katika utakatifu, Barua ya Mtume Paulo, (1 Th 04:03): utakatifu huonyesha uso wa kweli wa Kanisa, fanyeni waingie " leo "katika Mungu wa milele'".
Papa alimalizia hotuba yake na maoni kwamba, Mwaka wa Imani aliouzindua Jumatano,ni njia nzuri zaidi katika kukumbuka na maadhimisha Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican,, kama kiini cha mkazo wa ujumbe uliotolewa na Baraza hilo, ambao ni ujumbe wa imani katika Kristo, Mkombozi pekee wa dunia, anayeendelea kutangazwa na Mama Kanisa hata katika nyakati zetu. Hata leo, hilo bado ni muhimu na jambo la lazima , kuasiki upendo wa Mungu kwa watu wote wake kwa waume kila mahali na kila mfumo wa maisha na kila nyakati.
Papa ameonyesha tumaini lake kwamba, Makanisa yote, hasa katika maadhimisho ya mwaka huu, itakuwa ni nafasi muhimu kurudi katika chemichemi hai ya Injili, kubadilisha maisha na kukutana ana kwa ana na Yesu Kristo.








All the contents on this site are copyrighted ©.