2012-10-12 08:03:04

Jimbo kuu la Mwanza kuadhimisha kumbu kumbu ya matukio makuu ya kihistoria kwa hija, kesha na Ibada ya Misa Takatifu


Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, anawaalika kwa namna ya pekee waamini na watu wote wenye mapenzi mema katika kushiriki kwa umakini mkubwa maadhimisho ya kumbu kumbu ya ujio wa Mwenyeheri Baba Mtakatifu Yohane wa Pili Jimbo kuu la Mwanza kunako mwaka 1990. RealAudioMP3
Tukio hili linaloijumuisha Familia ya Mungu Jimbo kuu la Mwanza, litaanza kwa hija ya waamini kuelekea Kawekamo hapo tarehe 15 Oktoba, 2012 majira ya jioni, tukio litakalofuatiwa na mkesha wa sala na hatimaye kuhitimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu hapo tarehe 16 Oktoba 2012.

Ibada ya Misa Takatifu inalenga kuomba neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakati huu Jimbo kuu la Mwanza, linapoweka kwa mara ya kwanza katika historia ya uwepo wake, Jiwe la Msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kanisa kuu la Jimbo kuu la Mwanza, ndoto ambayo imeendelea kuhifadhiwa mioyoni mwa Familia ya Mungu kwa takribani miaka hamsini iliyopita.








All the contents on this site are copyrighted ©.