2012-10-11 11:00:40

Maonesho ya vitabu yafunguliwa Ujerumani


Kitengo cha Uchapishaji cha Vatican, kwa mara nyingine tena kinashiriki katika Maonesho ya Vitabu, yaliyofunguliwa rasmi huko Frankfurt, Ujerumani kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 14 Oktoba, 2012. Kitengo hiki kinashirikisha zaidi ya vitabu elfu sita. Katika banda la Vatican kuna machapisho pia kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani.

Machapisho kuhusu Mwaka wa Imani uliozinduliwa rasmi na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 11 Oktoba 2012 yana umuhimu wa pekee katika maonesho haya. Kuna vitabu vinavyozungumzia pia Uinjilishaji mpya, maisha ya kiroho na tafakari za kina zinazotolewa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.









All the contents on this site are copyrighted ©.