2012-10-11 15:56:47

Askofu Mkuu wa Canterbury aihutubia Sinodi


Askofu Mkuu Dr. Rowan Williams, Mkuu wa Jumuiya ya Waanglikani Duniani, Jumatano jioni, alihutubia Sinodi na alizungumzia changamoto za uijilishaji mpya, katika mtazamo wa Kanisa la Kianglikan. Pia aliangalisha umuhimu wa kutazama kwa makini msaada unaohitajika kutolewa wka watu ili wagundue uzuri wa imani ya Kikristu.
Kwenye hotuba yake , aliangalisha katika maandishi ya baadhi ya waandishi Mashuhuri Katoliki na wanateolojia , wa tangu kipindi cha Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican na kueleza kwamba, ongezeko la mashaka na ukana dini duniani na mifumo ya kifedha na utamaduni wa matangazo , vinahimiza kutafakari majibu yaliyotolewa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na waandishi hao mashuhuri.
Na kwamba , kipengere hiki cha kuhuisha upya imani yaKikristu , klicho tajwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican , ni hoja msingi inayotakiwa kutekewelezwa ili kwamba utangazaji wa Injili uweze kuwa na kishindo cha kuifikisha Injili ya ubinadamu kwa watu wote waliumbwa na sura ya ubinadamu wa Kristu. Kwa maana hiyo , Imani Katoliki na Ukstu kwa ujumla unawasilisha ubinadamu wa kweli.
Na hatuwezi kusahau kwamba, Mungu hhuonekana kwa kutazama jirani , na hilo ndilo jibu pekee linalotakiwa kuwasilishwa dunaini kote , kumpenda jirani katika mifumo na mipango yote ya kifedha na utendaji wake. Na kuishi kwa makini kunamaanisha kuzamisha mabadiliko ya ndani , kwa mana ya kujifunza kuhudumia wengine kwa imani, uaminifu na upendo. Na hivyo haki inakuwa ni tabia ya Ukristu.
Na kwamba, kwa wale wenye ufahamu mdogo juu ya mifumo na hierekia ya kanisa leo hii, mara nyingi huvutiwa na changamoto za maisha ya haki na tafakari za upendo unaonyesha sura ya Mungu.
Na kwa namna ya kipekee alitaja kazi maalum na shuhuda za kuonekana kama maisha ya Taize na Bose,au mifumo ya utendaji kama ile ya jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Focolare au chama cha Usharika na uhuru, akisema hutoa onjo jipya katika imani ya Kikristu .
Askofu Mkuu Dr Rowan Williams, anahudhuria Sinodi hii kama mgeni mwalikwa maalum wa Papa . Askofu Mkuu Rowan anatazamia kuachia cheo cha kuiongoza Jumuiya ya Waanglikan Duniani mwishoni mwa mwaka huu. Na mara kwa mara, ametembelea Roma na Vatican.
Pia ameutumia muda huu wa sinodi kuangana na Papa Benedikto XVI, Alhamsi hii, kuadhimisha Ibada ya Misa kwa ajili ya Ufunguzi wa mwaka wa Imani na sherehe ya miaka 50 ya kuzinduliwa kwa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.