Jumanne Asubuhi, mbele ya Papa na Maaskofu kutoka dunia nzima, Sinodi ilifunguliwa
na wito wa amani Syria. Na pia kuliwasilishwa matatizo yadhuluma kwa wahamiaji na
umuhimu wa kuchunguza dhamiri ya Kanisa, na njia za kuiishi imani.
Wajumbe
wa sinodi, wakitazama changamoto dhidi ya uinjilishaji mpya, waliomba msaada wa
kulindwa kwa wakimbizi na makundi madogomadogo dhidi ya aina fulani ya ubaguzi katika
jamii na kuwezesha ushirikiano na utunzaji wa utambulisho wao wa Kikristu
Sinodi
pia ilikosoa madhulumu yanayofanywa na makuhani na kuomba uchunguzi wa kidhamiri katika
mna za kuishi na kuwa mashahidi wa imani duniani na katika kuonyesha maana halisi
ya sakramenti katika uinjlishaji mpya, mkitajwa hatari za urasimu katika maisha ya
kisakramenti kwamba huhatarisha imani kupotea. Ni muhimu basi,Uinjilishaji mpya wa
Kanisa ufanyike kwa uneynyekevu mkuu na si katika mitazamo ya kujifungia katika mijadala
ya ndani ya makanisa , lakini kuitagaza Injili kwa unyenyekevu , katika mwanga wa
huduma mpya.
Pia ni muhimu kwa watumishi wa kanisa waliochukua dhamana ya
ukuhani, kujiepusha au kurudia kashfa za madhulumu hasa kwa wau wanyonge kama watoto,
na kupambana na vipingamizi vingine, kama haja ya kidharura, kupitia njia ya uelimishaji.Sinodi
imeonya ni wazi hakuna uinjlishaji kama muinjilishaji mwenyewe anaishi kinyume cha
Injili anayoitangaza.
Na Jumanne mchana, Maaskofu walisikiliza ripoti zilizowasilishwa
kutoka mabara matano, zikionyesha jinsi mandhari ya uinjilishaji mpya , imepokelewa
duniani kote. Kwa ujumla ripoti hizo zilionyesha kuwa na tatizo linalofanana changamoto
ya utandawazi, ambao imekuwa na mwelekeo wa kubadilisha tamaduni mahalia na kudharirisha
maadili ya kijadi, kama familia.
Na kwa namna ya pekee zilitazamwa kazi
za uinjilishaji barani Asia, kama hitaji msingi na si doto ya kufikirika katika kuzitazama
hali halisi za maisha ya Wakristu na jamii kwa ujumla kitamaduni, kihali na kidini,
ikiwa ni pamoja na kushughulikia mateso ya kishujaa ya wanaoiishi imani yao ya Kikristu.
Afrika, kwa upande wake, mapambano dhidi ya ubabe wa waislamu wasiovumilia
wengine, yalitazmwa kwa makini, ikiwemo mafundisho ya Papa Paulo VI, yaliyowataka
" Waafrika, kusimamam imara na kujiijilisha wenyewe kwa wenyewe". .