Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akiwahutubia mahujaji na wageni , waliofika kumsikiliza
Jumatano hii mjini Vatican, aliyarejea matukio mawili yanayozinduliwa wiki hii , yanayokwenda
sambamba, kufunguliwa kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican
na kuanza kwa mwaka wa Imani. Papa akiwa mmoja wa Mababa walioshiriki Mtaguso
Mkuu wa Pili wa Vatican, amezikumbuka vyema, shauku, tumaini na furaha, si tu ya
Maaskofu, lakini ya Kanisa zima Katika kipindi hicho. Ameonyesha tumaini lake
kwamba, tunapoanza Mwaka wa Imani, unao zinduliwa Alhamis hii 11 Oktoba 2012, inakuwa
ni muhimu kurejea nyaraka za mkutano huu muhimu, kama alivyoeleza Mwenye Heri Yohana
XXIII, kutangaza ukweli wa imani, kwa njia mpya , bila kubadili maudhui yake. Aliendelea
kufundisha kwamba, nyakati hizi zetu zilizomsahau Mungu, kunahitaji kukumbusha tena
ujumbe mkuu wa Baraza, kwamba, Ukristo ni imani kwa nafsi tatu za Mungu mmoja, Baba
Mwana na Roho Mtakatifu. Na ni kukutana kama mtu binafsi au jumuiya na Kristu
, mwenye kubadili na kutoa maana ya maisha . Mengi yote hutoka kwake. Papa aliomba,
kama ilivyokuwa wakati wa Baraza, pia katika wakati wetu huu, tuweze kutambua kwa
uwazi kwamba, Mungu yupo , na anatuangalia , na kutujibu , na wakati binadamu anapomsahau
Mungu, husahau jambo muhimu katika ubinadamu wake mwenyewe. Hivyo basi Maadhimisho
ya miaka hamsini wa Mtaguzo Mkuu wa Pili, na yanakumbusho hilo kwamba, Kanisa, na
waamini wake wote, wana wajibu wa kueneza ujumbe wa upendo wa Mungu wa kuokoa, unaoongoza
katika Heri ya milele.