Mababa wa Sinodi kwa ajili ya Uinjlishaji Mpya, wanaendelea kushirikishana hali halisi,
na uzoefu na ushauri kutoka maeneo yao, kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa. Jumatatu
kati ya waliohutubia sinodi ni muadhama, Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo
Kuu la Dar es Salaam, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki
Afrika na Madagascar,SECAM, alizungumza kwa niaba ya mabaraza hayo. Kardinali
aliitoa muhtasari wa historia ya Uinjilishaji Afrika akisema , historia inathibitisha
Uinjilishaji barani Afrika ni tangu mwanzo wa Kanisa, "Matendo ya Mitume ; 8,26, 39,
mnatajwa uinjilishaji uliofanywa na Philipo nchini Ethiopia. Ingawa Ukristu uliingia
mapema Kaskazini mwa Afrika, juhudi hizo hazikujipenyeza kwa haraka katika eneo la
Kusini mwa Afrika. Na hivo kwa wakazi wa Kusini mwa Afrika, inaweza kwao kuwa vigumu
kutambulisha kati ya Uinjilishaji mpya na uinjilishajiwa zamani. Hata hivyo bado inafaa
kuzungumzia Uinjilishaji mpya kwa Afrika, kwa kuanza na changamoto zilizotajwa na
Papa Paulo V1 mwaka 1969, aliyewataka Waafrika kujiinjilisha wenyewe .Pamoja na kupita
kwa miaka bado , hata leo wito huo kwa Kanisa Afrika, unahitaji kuitikikiwa kwa kishindo.
Ni wito kwa Makanisa Afrika kujenga ukomavu katika kazi hii ya kuinjilisha.
Ili
kutoa jibu kwa changamoto hii, Kanisa Afrika liliona umuhimu wa kuwa na mfumo wa
mmoja wa kichungaji ngazi za kitaifa na kimkoa, kwa ajili ya uhamasishaji mpya kwa
kazi hii ya uinjilishaji . Na hivyo Kanisa lilianzisha SECAM, mwaka 1969, kwa lengo
la kukuza na kudumisha umoja, katika ushirikiano na utendaji wa pamoja kwa Mabaraza
yote ya Afrika na visiwa vinavyozunguka Afrika. Udumishaji wa juhudi hizo zenye kuhamasisha
kazi za kichungaji leo hii, imekuwa ni wajibu wa waaamini wote wa waafrika, Maaskofu,
Mapadre, Watawa wanawake kwa wanaume, na makatekista na walei.. Na kati ya kazi
za kuonekana katika juhudi hizi za uinjilishaji mpya ni uanzishwaji wa jumuiya dogodogo
za Kikristu ambazo zimekuwa vituo hai vya uinjilishaji wa kina katika maisha ya kila
siku ya kanisa barani Afrika. Kardinali Polycarp Pengo, pia aliangalisha katika
changamoto zinazokwamisha uinjilishaji na uzamishaji wa imani barani Afrika . Kati
ya changamoto hizo ni mmomonyoko wa maadili ya utamaduni wa mwafrika, kunakotokana
na kasi yamwingiliano wa tamaduni kutoka nje katika mfumowa utandawazi. Na hivyo
inakuwa vigumu kwa Wakristu barani Afrika kupambanua kati ya mambo ya kipagani ya
nchi za nje na hasa Ulaya na Ukristu . Na kumekuwa na mwelekeo wa Ukristo kuchukuliwa
pia kama utamaduni wa kigeni. Aidha thamani ya utamaduni mahalia kuheshimu maisha
unapambanishwa na utendaji wa nchi za magharibi usio thamini maisha. Pamoja na changamoto
nyingi toka nje zinazodharirisha maadili ya mwafirika, inakuwa vigumu kwa watu mahalia
kupata utambuzi wa ukweli wa maisha. Kardinali Pengo aliendelea kutaja maovu yanayodharirisha
kazi za Uinjilishaji , ikiwemo udhaifu wa kurubuni haraka na kuingia katika mizozo
na machafuko ya kikikabila yenye kujirudiarudia, maradhi, usafirikshaji haramu
wa watu, mauaji ya kinyama na madhulumu kwa watoto na makundi madogomadogo manyonge
kama wanawake . Pia ameitaja changamoto nyingine inayokabili uinjilishaji barani
Afrika ni utendaji wa Waislamu wasiovumilia wengine. Katika hili, uinjilishaji umekuwa
ni mgumu hasa uwepo wa majadiliano wazi , katika maeneo yenye kuwa na Waislamu wengi.
Sehemu hizo makundi madogomadogo kiimani, hutenda kwa unyamavu mwingi na huishi
na hofu za kushambuliwa iwapo watajaribu kueneza imani yao. Na waislamu hao wasiovumilia
wengine, hawako tayari kusikiliza wengine na kuukubali ukweli . Hivyo, Uinjilishaji
mpya barani Afrika , unahitaji wainjilishaji waliokomaa katika imani, kutimiza
zaidi ya wito wa Paulo V1, kwamba waafirika ni lazima kujiinjilisha wenyewe, kama
inavyoonekana sasa kwamba , kuna Waafrika wamisionari katika mataifa ya magharibi,
Marekani na Ulaya. Pia kujali kwamba, katika juhudi hizo za kwenda kuinjilisha
nje ya Afrika, zisiwe na sababu za kujitafutia faida binafsi kwa mgongo wa Kanisa
na uinjilishaji wa kweli. Kwa kuzingatia yote haya , Sinodi kwa ajili ya Uinjilishaji
mpya, ni tukio linalopokelewa kwa mikono miwili hata barani Afrika. Ni kama ulivyo
wito wa Papa Benedikto XV1, kwa Afrika , kusimama imara na kuuchukua mkeka na kutembea
(Afrika Munus No. 148) Na kwa kufanywa upya katika imani, kupitia sinodi hii,
Kardinali Polycarp Pengo ameonyesha imani yake kwamba , Afrika itaweza kupambana na
changamoto zake kwa ushupavu zaidi leo hii. Kwa kuangaziwa na nyaraka mbili za
matokeo ya Sinodi maalum kwa Afrika, ”Kanisa barani Afrika ya mwaka 1995” na waraka
wa ”Dhamana ya Afrika , 2011” na pia Kateksimo ya Kanisa Katoliki, na hati yenye ufupisho
wa mafundisho sadikifu ya Kanisa , Kanisa la Afrika linatazamia mambo mengi mazuri
kutoka sinodi hii ya Unjilishaji mpya-