2012-10-09 15:25:15

Uijilishaji unahitaji, kwanza muumini awe na moto wa ndani wa Mungu ,ili apate ushupavu wa kuwainjilisha wengine -Papa


Baba Mtakatifu Benedikto XVI, Jumatatu akiuhutubia kikao cha kwanza cha Baraza la 13 la Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu, alizungumzia mambo mawili msingi; kwanza ni mapenzi ya kumtagaza Kristu duniani na pili ni ufahamu kwamba , Mungu hutenda ndani ya Kanisa. Baraza hilo linaloongozwa na Mada mbiu: Uinjilishaji Mpya kwa ajili ya kueneza Imani ya Kikristu.
Baba Mtakatifu alitaja hoja ya kidharura leo hii , ni kuelimisha uwepo wa Mungu kweli, kama ilivyokuwa siku za nyuma. Kuufahamisha ulimwengu kwamba, Kwa neno la Injili , Mungu aliuvunja ukimya, na kuzungumza na binadamu na kuingia katika historia ya watu. Kupitia Yesu Kristu, Neno lililomwilishwa, Mungu aliuonyesha upendo wake wote kwa binadamu kwa kukubali kuteseka hadi kifo na kufufuka.

Hilo ndilo jibu la Kanisa katika dharura hii muhimu ya kuinjilisha. Utume huu, unamhitaji muinjilishaji yeye mwenyewe kwanza, awe na moto wa ndani wa Mungu, ili aweze kuuwasha kwa ushupavu duniani. Wainjilishaji wenyewe wanatakiwa kuwa na utambuzi wa kiroho kwamba Mungu yumo ndani ya kanisa na anapenda kuwafikia watu wote duniani.

Pamoja na msisitizo huo, Papa alihoji , kwa namna gani utume huu unaweza kufanikishwa? Au ni mbinu zipi zinazofaa kuufikisha ukweli huu kwa watu wote, wake kwa waume wa nyakati zetu, ili waweze kufahamu habari za ukombozi wa kweli? Papa aliasa, hakuna sababu ya kuongopa kwa kuwa Kanisa huundwa na Mungu na binadamu kazi yake ni kuitambulisha kazi ya Mungu kwa wasiofahamu. Kanisa halikuanza kwa utendaji wa binadamu, bali kwa utendaji wake Mungu na Neno lake.
Papa alieleza na kutafakari juu ya ujio wa Yesu duniani akisema, historia inabaki daima katika ukweli wake kwamba, usiku mmoja huko Betlehemu , mtoto alizaliwa na kuibadili historia ya binadamu. Ni yuleyule aliyeteswa na kuuwa na kufufuka miaka elfu mbili iliyopita.

Papa akilitafakari tukio la Pentecoste, jinsi Mitume walivyopokea Roho Mtakatifu wakiwa wamejifungia katika Chumba cha Juu. Alilinganisha tukio hilo na Mitume na Baraza la sinodi hii iliyoanza na sala, akisema si tu kama ni utaratibu , lakini sala hizo ni ushuhuda ha, katika utambuzi kwamba, juhudihizi ni kutoka kw Mungu Mwenyewe.

Wao ni watendaji na kanisa na wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na Mungu. Kwa utambuzi huo , ni lazima wajikite katika uongofu au kwa maneno mengine, kuwa mashahidi wa Bwana wao hata katika hali za hatarishi. Papa alitaja dai hili kuwa ni suala nyeti kiasi kwamba, katika hali ngumu na hatarishi, dhamana inabaki kuwa uthabiti wa imani, moyo ulio tayari hata kuyatolea maisha kwa ajili ya imani.
Na kwamba, uongofu huu, unahitaji kuonekana kwa matendo, ni kama kuvaa nguo . Na hili ni suala la upendo ambao ni nguvu nyenye uwezo wote inayotakiwa kuwaka ndani ya mioyo ya Wakristu.
Papa alimalizia kwa kutahadharisha kwamba, kila Muumini ni lazima awe na mwali wa moto wa upendo wa Mungu ndani yake , mwali unaowaka katika maisha yake ya kila siku na kuwamulikia wengine . Hiyo ndiyo Roho ya uinjilishaji mpya. .








All the contents on this site are copyrighted ©.