2012-10-09 15:30:38

Radio Vatican kutumia facebook kueneza Injili kwa kizazi kipya


Hivi karibuni, kitengo cha Kiingereza cha Redio Vatican, kilizindua ukurasa mpya katika mtandano wa Facebook na hivyo kuiwezesha sauti ya Kanisa la ulimwengu na Papa kuzama zaidi katika ulimwengu wa tarakimu na mitandao ya mawasiliano jamii.

Mkuu wa Kitengo cha Idhaa ya Kiingereza Radio Vatican, Profesa Sean Patrick Lovett, ameeleza , kwa kutumia tovuti ya facebook, inayotumiwa na mamillioni ya watu, inakuwa ni nafasi nyingine kwa Radio Vatican, kuungana na mashirika mengine Katoliki yanayokwisha tayari kujiunga katika uwanja huu wa mawasiliano, ulioonekana kufaa kuifikisha Hbari njema ya Injili kwa watu wengi zaidi hasa lika la vijana. Pamoja na Kiingereza pia huduma hii ya uinjilishaji mpya katika facebook , inapatikana katika lugha ya Kireno, Kifaransa, na Kiarabu.

Profesa Sean Patrick Lovett, , ameendelea kutaja umuhimu wa kutumia Facebook , kwamba ni njia nyingine nyepesi ya kuufikisha ujumbe wa Injili kwa watu , kwa kuwa matumizi ya tarakimu katika dunia ya leo, hayawezi kukwepeka. Ndiyo mfumo uliotanda katika kupashana habari na ni utendaji wa kisasa katika mawasiliano. Kupitia ukurasa huu wa Facebook, watumiaji wataweza kupata habari mpyampya za matukio ndani ya Vatican na kusikiliza hata sauti za wahusika.
Profesa Sean Lovett, ametaja lengo kuu katika juhudi hizi ni kujaribu kuwataarifa watu kwa kina kinachotokea katika kanisa la Ulimwengu na duniani kwa ujumla. Na kwamba, kuzinduliwa kwa ukurasa huu sambamba na kuanza kwa Baraza la Sinodi ya Maaskofu si ajali lakini ni mahali ni pake maana Sinodi pia inalenga katika kufanikisha uinjilishaji mpya duniani . Hivyo ni kuwapa watu nafasi zaidi za kuuupata ujumbe wa Neno la Mungu , hasa kwa lika la vijana.








All the contents on this site are copyrighted ©.