2012-10-08 08:25:28

Papa kutoa Rehema kamili kwa watakao shiriki kikamilifu matukio ya mwaka wa Imani


Wakatoliki watakao shiriki au kufuatilia kwa makini matukio yanayohusiana na mwaka wa Imani , wataweza kupata rehema maalum.
Hati Vatican iliyotiwa sahihi na Kardinali Manuel Monteiro de Castro, Mkuu wa kitengo cha Kitubio na Askofu Krzysztof Nykiel, Mjumbe wa Kitume katika Kitengo cha Kipapa cha Kitubio, imetaja azimio hili kwamba, Papa ameidhinisha rehema kamili kwa waaamini, watakao shiriki kikamilifu matukio ya kikanisa yatakayofanyika wakati wa mwaka wa Imani, unaoanza Octoa 11 2012 hadi 24 Novemba 2013. Na maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya ufunguzi wa Mtaguso Mkuu w Pili wa Vatican.

Baraka hizi zitawafikia wale ambao watatimiza nia za kuutolea mwaka wa imani, kwa ajili ya uongofu wa kweli, wakipania kujirekebisha , kusoma au kufanya tafakari makini juu ya utendaji wa Mtaguso Mkuu wa Pili , na vipengere vilivyoelezwa katika Kateksimu Katoliki.

Waraka huo umetaja lengo msingi la Mwaka wa Imani kwamba, ni "kufanya majiundo mapya yenye kutafuta kuishi maisha matakatifu kwa kadiri inavyowezekana hapa duniani. Na Rehema kamili hutolewa na Papa kwa waaamini wanaougama na kufanya toba kwa uaminifu, na kuadhimisha Ibada za Ekaristi na kutolea sala kwa mujibu wa nia za Papa ".

Waraka huo unabaini kwamba, Pia rehema zitatolewa kwa wale watakaofanya hija katika Madhabahu Matakatifu. Na pia kwa waamini ambao hawawezi kuondoka katika makazi yao na kwenda kushiriki Ibada Kanisani , kutokana na udhaifu wa mwili mfano maradhi au sababu zingine msingi, pia bado wanaweza kupokea rehema kwa kufuatilia matukio ya mwaka wa imani na Ibada zitakazoongozwa na Papa, ikiwemo kusikiliza mahubiri ya Maaskofu kupitia njia ya redio au televisheni, kujisomea Kateksimu na nyaraka zingine muhimu za Kanisa na kufanya tafakari wakikamilisha kwa sala ya Baba Yetu , Nasadiki na kuomba msaada wa Bikira Maria na mitume au Watakatifu wasimamizi wao. .








All the contents on this site are copyrighted ©.